Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

vivutio hivi kimoja baada ya kingine, vinavyopatikana kaika hifadhi hii muhimu.

Mto Tarangire
Mto huu ambao unaingia hifadhini ukitokea katika miinuko ya Kondoa iliyopo upande wa Kusini Magharibi, unatiririsha maji yake kuelekea upande wa Kaskazini mwa hifadhi hii kabla ya kutoka nje ya hifadhi kwa upande wa Kaskazini Magharibi mwa hifadhi hii kubwa. Mto Tarangire unajulikana sana hasa kipindi cha ukame ambapo husaidia sana kutunza maelfu ya wanyamapori na viumbe hai wengine waliopo katika eneo hili la hifadhi.
 
Vile vile kutokana na uwepo wa mto huu kuendelea kuwa na maji mengi hadi kipindi cha ukame, idadi kubwa sana ya wanyama husogea maeneo ya karibu na mto huu, hasa sehemu za Kaskazini mwa hifadhi hii. Hii ndio sehemu nzuri ya kuona wanyama wengi na wa kila aina, kama vile makundi makubwa ya tembo na wanyamapori wengine. Kwa hiyo mto huu ni muhimu sana kwa maisha ya viumbe hai wa hifadhi hii, mimea na wanyama.
 
Miti ya Mibuyu
Mibuyu, au miti ya mibuyu ndio miti inayoonekana zaidi katika hifadhi hii ya Tarangire, mibuyu ni miti mikubwa sana kwa umbo, ni miti yenye historia ya kipekee kwa uwezo wake wa kuishi na kuendelea kuwepo kwa zaidi ya miaka 1000, katika hifadhi hii ya Tarangire utajionea miti hii ya ajabu sana, ni miti inayotunza maji sana, na ni miti inayostahimili ukame sana, hivyo mara nyingi miti hii huota au huweza kuonekana zaidi sehemu zenye ukame.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…