Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

b95dfe3f07daa07e82206470b9f370f1.jpg
Logo ya kijanja kwa wajanja
 
.Hifadhi ya Taifa ya Tarangire ipo upande wa Kusini Mashariki mwa Ziwa Manyara. Hifadhi hii yenye ukubwa wa kilomita za mraba 2,850 inaweza kufikika kwa urahisi kutoka Arusha kupitia barababra nzuri kabisa. Mto Tarangire unaotiririsha maji mwaka mzima kuelekea upande wa Kaskazini mwa hifadhi hii ndio umeipa hifadhii hii jina hilo. Kwa sababu ya uwepo wa mto huu katika kipindi chote cha mwaka, umekuwa msaada mkubwa sana kwa maisha ya wanyamapori ndani na nje ya hifadhii hii.
 
vivutio hivi kimoja baada ya kingine, vinavyopatikana kaika hifadhi hii muhimu.

Mto Tarangire
Mto huu ambao unaingia hifadhini ukitokea katika miinuko ya Kondoa iliyopo upande wa Kusini Magharibi, unatiririsha maji yake kuelekea upande wa Kaskazini mwa hifadhi hii kabla ya kutoka nje ya hifadhi kwa upande wa Kaskazini Magharibi mwa hifadhi hii kubwa. Mto Tarangire unajulikana sana hasa kipindi cha ukame ambapo husaidia sana kutunza maelfu ya wanyamapori na viumbe hai wengine waliopo katika eneo hili la hifadhi.
 
Vile vile kutokana na uwepo wa mto huu kuendelea kuwa na maji mengi hadi kipindi cha ukame, idadi kubwa sana ya wanyama husogea maeneo ya karibu na mto huu, hasa sehemu za Kaskazini mwa hifadhi hii. Hii ndio sehemu nzuri ya kuona wanyama wengi na wa kila aina, kama vile makundi makubwa ya tembo na wanyamapori wengine. Kwa hiyo mto huu ni muhimu sana kwa maisha ya viumbe hai wa hifadhi hii, mimea na wanyama.
 
Miti ya Mibuyu
Mibuyu, au miti ya mibuyu ndio miti inayoonekana zaidi katika hifadhi hii ya Tarangire, mibuyu ni miti mikubwa sana kwa umbo, ni miti yenye historia ya kipekee kwa uwezo wake wa kuishi na kuendelea kuwepo kwa zaidi ya miaka 1000, katika hifadhi hii ya Tarangire utajionea miti hii ya ajabu sana, ni miti inayotunza maji sana, na ni miti inayostahimili ukame sana, hivyo mara nyingi miti hii huota au huweza kuonekana zaidi sehemu zenye ukame.
 
Tafiti za masuala ya ikologia ya miti wanasema miti hii ya mibuyu iliyopo Tarangire mingi ina zaidi ya miaka 1000; hivi kwenye maisha yako ulisha wahi kuona kiumbe hai chenye umri zaidi ya miaka 1000. Jibu lako ni hapana. Sasa hapa ndio sehmu pekee unaweza kuona maajabu haya ya miti ya mibuyu.
 
Maficho ya majangili
Maficho haya ni kama pango ambalo walitumia miaka ya nyuma sana, kama sehemu ya kujificha na kujihifadhi. Maficho haya yapo ndani ya mti wa mbuyu ambao ni mti mkubwa sana kuliko miti yote ya hifadhi ya Tarangire, pango hili linakadiriwa kuwa na zaidi ya miaka 300. Uwazi uliopo kwenye mti huu wa mbuyu ni zaidi ya kipenyo cha mita kumi.
 
Ndani ya maficho/pango hili lina uwezo wa kuchukua au kuhifadhi zaidi ya watu 20, ambao wengi waliotumia eneo hili ni wawindaji. Ni sehemu nzuri sana ya kutembelea na kuona ili upige picha na kujionea ukuaba wa pango hili lililopo ndani ya mbuyu.
 
Makundi makubwa ya tembo
Hifadhi ya tarangire ina makundi makubwa sana ya tembo, kipindi cha ukame (dry season), hifadhi hii inakadiriwa kuwa na tembo zaidi ya 4000 na 6000, lakini tembo wengi zaidi wanaweza kuonekana kipindi cha mvua. Karibu sana utembelee hifadhi hii nzuri.
 
Ndege
Hifadhi ya Taifa ya Tarangire ina zaidi ya jamii 550 za ndege ambao ndio wamejulikana, na kati ya ndege hao baadhi yao wapo katika tishio la kutoweka. Tafiti zinaonyesha kwamba kipindi cha mvua ndio kipindi kizuri sana kwa aina nyingi za ndege kwenye eneo hili kuzaliana kwa wingi. Mabwawa na mito iliyopo katika hifadhi hii yanakuwa ndio sehemu nzuri zaidi ya kuona ndege wengi sana. Vile vile uoto wa asili katika hifadhi hii ndio unaopelekea wingi wa ndege katika eneo hili.
 
Mabwawa
Katika hifadhi ya Tarangire kuna mabwawa makubwa na mapana sana, ambayo ndio sehemu kuu ya vyanzo vya maji kwa sehemu za hifadhi hii, mabwawa haya husaidia kusambaza maji sehemu za Kaskazini za hifadhi hii hadi kwenye ziwa Burunge ambalo ni ziwa la msimu. Mabwawa ni sehemu muhimu sana ya hifadhi yoyote, kwani husaidia wanyama wengi hasa kipindi cha ukame, wanyama kama tembo na nyati hupenda sana maji.
 
Vichuguu vya mchwa
Kila kitu ndani ya hifadhi kina maana na kusudi lake, uwepo wa vichuguu hivi imekuwa ndio makazi salama ya wanyama wadogo wanaokula nyama kama vile ng’uchiro, (mongoose), vichuguu hivi vilivyo achwa ndio vinavyo ipendezesha sana hifadhi hii ya Tarangire. Mwonekano wa vichuguu hivi ni muhimu kwa wageni kuweza kuwaona wanyama, pia utawakuta wanyama hawa wadogo wakicheza na kujificha kwenye mashimo madogo madogo yaliyopo ndani ya vichuguu hivi.
 
Ni hifadhi ambayo kwa kingereza wanasema where the beach meets the bush, akimaanisha kwamba ni hifadhi ambayo ufukwe wa bahari unakutana na hifadhi. Ni hifadhi ambayo ipo upande wa Mashariki mwa nchi yetu.

Hifadhi hii ambayo ilianza kama Pori Tengefu (Game Reserve) tangu miaka ya 1960, baada ya hapo hifadhi hii ilipandishwa kutoka kuwa Pori Tengefu hadi kuwa Tifadhi ya Taifa ya Saadani mnamo mwaka 2005, baada ya kupanuliwa kuongeza msitu wa Zaraninge na Ranch ya Mkwaja. Hifadhi hii yenye ukubwa wa kilomita za mraba 1,100, ni hifadhi ambayo ilikuwa na matukio mengi ya ujangili kwenye miaka ya 1990, lakini baadya ya juhudi za makusudi hali hii imebadilika kabisa
 
kwa sasa ndani ya hifadhi hii unaweza kuona makundi ya wanyamapori kama tembo, nyani, ngiri, simba, twiga, swala, fisi na hata chui. Ni hifadhi ya kipekee inayopakana na bahari ya Hindi kwa upande wa Mashariki, ambapo watu wa Pwani ndio wanaoishi karibu zaidi na hifadhi hii, mfano Tanga, Bagamoyo, na hata Dar es salaam. Ni hifadhi yenye vivutio vingi vya tofauti kabisa na hifadhi nyingine za Tanzania kutokana na mambo mengi hasa utamaduni wa watu waishio karibu na hifadhi hii.
 
Hii ni hifadhi ambayo inafikika kwa urahisi na watu wengi, na pia ni hifadhi inayofikika kila wakati au kila msimu wa mwaka, yani kuwe na mvua au kusiwe na mvua unaweza kufika katika hifadhi hii kipindi chochote cha mwaka. Kwa hiyo ni hifadhi ambayo kama upo Dar es salaam, Tanga, au mikoa ya karibu kama Bagamoyo, Pwani, unaweza kutembelea hifadhi hii kwa gharama nafuu sana. Na pia unaweza kutembelea na vivutio vingine vilivyopo hata nje ya hifadhi hii, vingi vikiwa ni vya kihistoria, kwa mfano Bagamoyo, na Makumbusho ya Dar es salaam.
 
Hii ni hifadhi ambayo inafikika kwa urahisi na watu wengi, na pia ni hifadhi inayofikika kila wakati au kila msimu wa mwaka, yani kuwe na mvua au kusiwe na mvua unaweza kufika katika hifadhi hii kipindi chochote cha mwaka. Kwa hiyo ni hifadhi ambayo kama upo Dar es salaam, Tanga, au mikoa ya karibu kama Bagamoyo, Pwani, unaweza kutembelea hifadhi hii kwa gharama nafuu sana. Na pia unaweza kutembelea na vivutio vingine vilivyopo hata nje ya hifadhi hii, vingi vikiwa ni vya kihistoria, kwa mfano Bagamoyo, na Makumbusho ya Dar es salaam.
 
Vivutio ambavyo unaweza kuviona katika Hifadhi hii ni vingi sana vikiwemo vya kihistoria na vya kitamaduni, kama vile maboma ya mawe yaliyojengwa na Wajerumani, hali nzuri ya hewa katika ufukwe wa bahari ya hifadhi hii ya Saadani, na mandhari nzuri sana ya ufukwe wa pwani ya bahari ya Hindi inayopakana na hifadhi hi kwa kiasi kikubwa, bila kusahau tamaduni za watu wa Pwani hasa kwenye mavazi, vyakula na hata kuongea.
 
Back
Top Bottom