kwa sasa ndani ya hifadhi hii unaweza kuona makundi ya wanyamapori kama tembo, nyani, ngiri, simba, twiga, swala, fisi na hata chui. Ni hifadhi ya kipekee inayopakana na bahari ya Hindi kwa upande wa Mashariki, ambapo watu wa Pwani ndio wanaoishi karibu zaidi na hifadhi hii, mfano Tanga, Bagamoyo, na hata Dar es salaam. Ni hifadhi yenye vivutio vingi vya tofauti kabisa na hifadhi nyingine za Tanzania kutokana na mambo mengi hasa utamaduni wa watu waishio karibu na hifadhi hii.