Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Pamoja mkuu
TI.jpg
 
NJIA RAHISI ZA KUTAMBUA JINSIA YA MTOTO ALIYEKO TUMBONI.

Mwanamke anapokuwa mjamzito huwa na wasi wasi na kushindwa kugundua kama ujauzito aliobeba ni mtoto wa kike au wa kiume. Kuna njia mbalimbali ambazo wakunga, wataalamu wa afya na wanawaake wazoefu huzitumia kutambua jinsia ya mtoto aliyeko tumboni ambapo mara nyingi asilimia zaidi ya 50 huwa ni kweli. Zifuatazo ni dalili na njia zinazotumika kutambua jinsia:-
Umeshawahi kufanyia uchunguzi hizi dalili na kujiridhisha?
 
FAHAMU KUHUSU KUVIMBA KWA BANDAMA(Splenomegaly)

Maambukizi na magonjwa mengi kwa muda mrefu husabisha kuvimba kwa bandama(spleen) ambayo iko kushoto mwa tumbo na hivyo kuharibu utendaji wake wa kazi kama kuondoa vimelea kwenye damu, kutengeneza kinga ya mwili, kuondoa chembe nyekundu zisizo na matumizi mwilini.
 
Ugonjwa huu usababishwa na maambukizi ya virusi, vimelea, bakteria, saratani ya damu, presha, magonjwa ya moyo, ugonjwa sugu wa ini, homa ya ini, upungufu wa damu n.k. Tatizo ili lisipotibiwa husababisaha maambukizi na magonjwa ya mara kwa mara, kuvuja damu na kupasuka kwa bandama.
 
DALILI
Maumivu makali ya kushoto mwa tumbo yanayoelekea mpaka kwenye bega la kushoto.
Maumivu au kichomi katika kifua tumbo au kibofu vinapojaa.
Maumivu ya mgongo.
Dalili za upungufu wa damu
Kushiba haraka hasa upande wa kushoto wa tumbo
Maambukizi ya mara kwa mara.
Kutokwa na damu mara kwa mara.
 
MATIBABU.
Baada ya kufanyiwa uchunguzi na vipimo vya utrasound, MRI au vipimo vya damu na kugundua uwepo wa tatizo ili mara nyini tiba yake huwa ni upasuaji na dawa au chanjo za kupunguza au kujikinga na maambukizi. Pia elimu hutolewa kwa ajili ya kuepuka mambo yanayoongeza presha tumboni kama mazoezi na michezo mikali yenye uwezekano wa kusababisha kuvuja au kupasuka kwa bandama.
Pia wagonjwa wanashauriwa kuvaa mkanda wanapoendesha gari ili kuepuka kupasuka kwa bandama iwapo itatokea ajali.
 
Mgonjwa anashauriwa kula vyakula vya asili asa matunda, mboga za majani na viungo ambavyo huongeza kinga ya mwili na kumkinga na magonjwa.
Epuka matumizi ya kahawa, nyama za mafuta, chumvi na sukari nyingi mwilini.
Epuka matumizi ya pombe, madawa, sigara na tumbaku.
Tumia juisi ya mshubiri, machungwa na papai mara mbili kwa siku husaidia kutibu tatizo ili.
 
KWA WANAOSUMBULIWA NA TATIZO LA KUVIMBA MIGUU.

Tatizo la kuvimba miguu husababishwa na kujikusanya kwa maji maji ambayo uvuja kutoka katika mishipa ya damu kutoka na sababu mbalimbali zinazosababisha damu ishindwe kurudi kwenye moyo kutoka katika miguu.
 
Hali hii huweza kutokea pia kwenye mapafu, ubongo, tumboni, na kwenye mapaja lakini kutikana na mvuto wa dunia huweza kuonekana zaidi kwenye vifundo vya miguu na bila maumivu.
Mambo yanayochangia na kusababisha tatizo ili mara nyingi huwa ni ujauzito, ugonjwa sugu wa ini, figo, ini na moyo kushindwa kufanya kazi, dawa za kupunguza mfadhaiko na shinikizo la damu.
 
MATIBABU YAKE.
Fika hosipitali kama kuvimba miguu inaambatana na kubanwa na kifua, kushindwa kupumua, maumivu makali ya kifua, kuna uvimbe wenye maumivu au joto kali, matatizo ya moyo, ini na figo ambapo dawa za kupunguza majimaji mwilini, kusaidia moyo, ini na figo kufanya kazi zitatolewa kwa kwa maelezo ya wataalamu wa afya.
Unaweza kufanya yafuatayo kujitibu mwenye kabla ya kumuona daktari
 
Nyanyua miguu yako juu ya usawa wa moyo wakati umelala kwa muda wa dakika 30 ili kuwezesha damu ya kutosha kurudi kwenye moyo. Fanya hivi walau mara 3 kwa siku kupata matokeo bora zaidi
Kufanya mazoezi laini pia itakusaidia kupeleka damu kwenye moyo na hivyo kurekebisha mzunguko wa damu
 
TATIZO LA VIDONDA MDOMONI



Vidonda mdomoni husababisha sana maumivu makali pamoja na kumfanya mtu asiweze kuongea vizuri na watu.Vidonda hivi husababishwa na kutafuta kwa muda mrefu hasa bigijii au kitu chochote, uvutaji wa sigara,maambukizi ya virusi, bakteria na fungasi sambamba na ukosefu wa madini na virutubisho vya folic, zinc, vitamin c,vitamin B12, na madini ya chuma.
 
Vidonda hivi huwaathiri sana watu wengi na hutokea sana kwenye lips, ulimi , mashavu, kingo na kuta za meno ambapo pia huweza kusambaa hadi kwenye koromeo endapo havitatibiwa mapema.


Pamoja na kutembelea hospitali ambapo dawa kama za antibiotiki, fangasi, virusi na zile za kupunguza maumivu na uvimbe huweza kutolewa kulingana na ukubwa wa tatzo pia unaweza kufanya yafuatayo kujitibu nyumbani
 
Back
Top Bottom