[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. Kuna kukoroma na kukoroma. Kuna watu wanakoroma mpaka nyumba inatikisika.
Na wengine wana sleep apnea. Wanakoroma halafu ghafla wanakata hata kupumua. Ubongo ukianza kukosa Oxygen ya kutosha ndo unawashtua na wanaripuka tena na kuendelea. Hii inahitaji tiba kwa sababu mushkeli kidogo tu ukitokea mtu anafia usingizini hata kama anaonekana ni mzima mwenye afya. Pia hawawezi kulala vizuri na mwili haupati Oksijeni ya kutosha. Matokeo yake mchana wanakuwa wamechoka na kusinzia sinzia ni kawaida.
Kukoroma pia kunatajwa kuwa ni dalili mojawapo ya matatizo ya moyo, na guidelines za mamlaka ya vyakula na madawa ya Marekani (FDA) inawataka wakoromaji sugu kuchunguza afya za mioyo yao mara kwa mara!