carbamazepine
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 46,577
- 285,648
ATHARI ZA KUCHANGANYA DAWA ZA HOSPITALI NA TIBA MBADALA/MITISHAMBA
ZINAENDELEA......
[emoji260][emoji260][emoji260]Mwingiliano
Dawa tunazotumia huathiri miili yetu kwa wema au kwa ubaya. Dawa zinapoingiliana kiutendaji zinaweza kupingana au kuongezeana nguvu na kuleta ufanisi au kuongeza makali ya dawa na kuwa sumu. Baadhi ya dawa za asili zitokanazo na mimea huongeza makali ya dawa za hospitalini na nyingine hupunguza makali yake na kuvuruga kazi iliyokusudiwa ya kupambana na vimelea vya magonjwa
Dawa za hospitalini pia huweza kuingiliana na zile za kufukiza, kupaka, kuchoma sindano au kuchanja.
Madhara vile vile hutegemea kiasi cha dawa, maandalizi yake, umri wa mgonjwa, jinsia, maumbile ya vinasaba na aina ya magonjwa aliyonayo.
[emoji264][emoji264]Mfano kama una matatizo ya figo na ini, ni rahisi sana kudhurika kwa mwingiliano wa utendaji wa dawa.
[emoji326][emoji326][emoji326]Mifano ya dawa zinazoingiliana
=Vitunguu saumu huingiliana na dawa za kupunguza makali ya VVU kama vile Ritonavir na Saquinavir.
Vitunguu saumu hupunguza nguvu ya dawa hizi kiasi kwamba mgonjwa anaweza kuwa na virusi vyenye usugu wa dawa hizo.
==Vitunguu swaumu, tangawizi, mbegu na majani ya mpapai pamoja na bizari pia huongeza hatari ya mwili kushindwa kugandisha damu vinapotumiwa pamoja na dawa za hospitali. Hii ni kutokana na kufanya damu kuwa nyepesi.
===Mshubiri (Aloe vera) unapotumiwa pamoja na dawa za moyo aina ya digoxin , huongeza hatari kwenye moyo kutokana na dawa hiyo asili kuwa na kawaida ya kuondoa madini ya potassium mwilini.
===Mshubiri una uwezo wa kusababisha mtu kupata choo laini au kuharisha na kupoteza madini ya potassium. Ili moyo ufanye kazi vizuri unahitaji kiasi cha kutosha cha potassium.
===Dawa za asili zitokanazo na Chamomile na Mpasheni zinaweza kuingiliana na dawa za usingizi za hospitalini na kuongeza hatari kwani nazo hufanya kazi ya namna hiyo.
[emoji326][emoji326]Dawa nyingi za asili zinaweza kuingiliana kiutendaji na dawa za kisukari, uzazi wa mpango na viuavijasumu. Hivyo ni muhimu kuchukua tahadhari kabla ya hatari.