Ukosefu wa lishe bora pia husababisha upungufu wa seli nyekundu za damu.
Ili kuzalishwa seli nyekundu za damu mwili unahitaji protini, kabohaidreti, vitamini B12, asidi ya foliki na madini ya chuma kwa wingi. Endapo mwili utakosa vitu hivi kwa ukosefu wa lishe bora mwili utashindwa kuzalisha seli nyekundu za damu.