Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ili kuwezesha mwili wako kufanya kazi kwa ufanisi na kuwa na kinga ya kutusaha ya mwili wako dhidi ya magonjwa huna budi kulinda kiwango cha damu ya mwili wako. Kupata lishe iliyo bora hasa vyakula vyenye protini, vitamini B12, madini ya chuma kwa wingi na asidi ya foliki vitakusaidia kuufanya mwili wako kutengeneza seli nyekundu za damu kwa ufanisi na seli nyingine katika damu.
 
Virusi ni vipande vya seli ambavyo hutegemea seli hai ili kukamilisha mzunguko wa maisha yake, mfano, kuzaliana na kupata virutubisho. Virusi vimekua tishio kubwa sana katika kizazi cha sasa kwasababu husababisha magonjwa mbalimbali na mengi imekua ni vigumu kuyatibu. Virusi vimekua ni vimelea vyenye uwezo mkubwa wa kujibadilisha kutokana na mazingira vilipo, na hii ndio sababu moja wapo inayofanya virusi kuendelea kua tishio na kusababisha kuibuka kwa magonjwa mapya.
 
Ugonjwa kama ukimwi ni mfano wa magonjwa yanayosabishwa na virusi na ndio ugonjwa mkubwa kwa sasa unaotikisa dunia. Pia kuna magonjwa kama Tetekuwanga, Polio, na magonjwa ya mlipuko kama Ebola nayo husababishwa na virusi.
Najua utakua unajiuliza maswali mengi kwa nini dawa ya virusi inakua ni vigumu kupatikana.
Kutokana na virusi kutokua na uwezo kuwa na maisha vikiwa nje ya selina hutegemea kila kitu kutoka kwenye seli. Hivyo basi ili kutambulika kama kirusi na kusababisha madhara lazima kiwe ndani ya seli. Kukiangamiza kirusi peke yake kikiwa ndani ya seli bila kuathiri seli yenyewe ni vigumu. Na kwa kuangamiza seli ya mwili iliyibebe kirusi husababisha madhara mengine katika mwili. Pia virusi vina tabia ya kujibadilisha badilisha muonekano wake, hivyo kuwa kungu kwa baadhi ya dawa kushindwa kukitambua.
 
Virusi vinaweza kusambaa kwa njia mbalimbali kama;
Kwa njia ya hewa
Baadhi ya virusi vina uwezo wa kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya hewa, hii husababishwa na mtu aliyeathirika na virusi kukohoa au kupiga chafya na mwingine aliyeko karibu nae kuvipata virusi kwa njia ya hewa.

Kwa kugusana
Hapa mtu anaweza kuambukizwa virusi kwa kumgusa mtu aliyeathirika, ieleweke kwamba sio tu kumgusa mgonjwa kunakusababishia kuambukizwa virusi bali hutegemea virusi hivyo vinapatikana wapi. Kuna baadhi ya virusi hupatikana kwenye mate, makamasi au kinyesi, hivyo basi endapo mgonjwa atakua amechafuka na moja kati ya hayo basi kumshika au kushika mate, makamasi au kinyesi cha mgonjwa huyo unaweza kuambukizwa.

Kwa njia ya damu.
 
Kuna baadhi ya virusi hutegemea hasa seli zilizopo ndani ya damu ili viweze kuishi na kusababisha madhara. Mfano, virusi vya ukimwi hutegemea seli nyeupe za damu. Hivyo basi virusi hivyo huweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya damu. Endapo damu yako na itakutana na damu ya mtu ambaye ameisha athirika na virusi utaambukizwa virusi hivyo.

Kwa ufupi bila shaka utakua umeelewa virusi ni nini, na tabia zake mbalimbali na njia ambazo virusi hivi vinaweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
 
😀😛Shikamoo Pesa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…