Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tottenham wapo tayari kupigana vikumbo na Chelsea majira ya joto kuiwania saini ya Ross Barkley, kwa mujibu wa Mirror .
Rekodi ya Mauricio Pochettino kuzalisha wachezaji kwa ajili ya Uingereza inaweza kuirahisishia Spurs mchakato huo, kwani Barkley anataka kupata nafasi Kombe la Dunia mwakani.
 
Real Madrid wanaandaa kitita cha €200 milioni kwa ajili ya straika wa Tottenham Harry Kane wanapotafuta mrithi wa kudumu wa Cristiano Ronaldo, kwa mujibu wa Don Balon .
Blancos wameona jinsi Ronaldo anavyohaha kutafuta magoli msimu huu, wakati wenzake wanaounda BBC Karim Benzema na Gareth Bale wakisumbuliwa na majeraha.
 
Chelsea wapo tayari kuamsha nia yao kumsajili mshambuliaji wa Arsenal na beki wa Juventus Alex Sandro, kwa mujibu wa Mirror .
Blues walimkosa mchezaji huyo wa Juventus majira ya joto, lakini bado miamba hao wa Italia hawajafikia makubaliano ya mkataba mpya na mchezaji wao.
 
AC Milan wanataka kumrejesha Antonio Conte Italia kutoka Chelsea msimu ujao wa majira ya joto, kwa mujibu wa Corriere dello Sport .
Bosi huyo wa Blues amekiri hadharani kuwa amepanga kurejea kwao Italia, na Rossoneri wameonyesha nia ya kumpeleka San Siro.
 
Bayern Munich wamefanya mawasiliano na kocha wa zamani wa Barcelona Luis Enrique, kwa mujibu wa Eurosport.de .
Miamba hao wa Bundesliga wanatafuta meneja mpya baada ya kumtupia virago Carlo Ancelotti na Luis Enrique ni miongoni mwa wanaopewa nafasi kubwa kuinoa klabu hiyo.
 
Manchester United watafanya jaribio la kumsajili Mesut Ozil kwa uhamisho wa bure msimu ujao wa majira ya joto, Jose Mourinho akiwa na tumaini kubwa la kuipata saini yake, kwa mujibu wa The Independent .
Mourinho alifanya kazi na Ozil akiwa Real Madrid na sasa anataka kumsajili Man United, Ozil atakuwa huru kuongea na klabu nyingine Januari.
Mkataba wake unaisha 2018 na hajaonesha kama anataka kubaki Emirates.
 
Chelsea na Manchester United zinamskauti beki chipukizi wa Middlesbrough Dael Fry, kwa mujibu wa Teamtalk .
Fry amejihakikishia nafasi kwenye kikosi cha Boro kwenye michauno ya Championship msimu huu na amezivutia klabu za Ligi Kuu Uingereza.
 
Arsenal wapo tayari kumuuza Mesut Ozil Januari, klabu ya Serie A Inter Milan ikiwa anatamani kuipata huduma ya Mjerumani huyo, kwa mujibu wa Mirror .
The Gunners hawapo tayari kumlipa Ozil kiasi cha paundi 350,000 anazotaka kwa wiki mkataba wake ukitarajiwa kufika tamati majira ya joto.
 
Chelsea wapo tayari kumlipa beki wa kushoto wa Napoli Faouzi Ghoulam €5 milioni kwa mwaka ili ajiunge na klabu hiyo uhamisho wa Januari, kwa mujibu wa Le Buteur .
Blues walimkosa Alex Sandro wa Juventus majira ya joto na bado wanatamani kuongeza beki wa kuimarisha safu yao ya ulinzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…