Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kumbuka hii ni tabia, haitakuwa rahisi, itachukua muda mpaka iwe tabia yako. Imekuchukua miaka mingi kuwa na tabia hizo ulizonazo. Wekeza muda na iweke kwenye matendo tabia hii mpaka utakapoona inaanza kukupa matokeo. Nakuhaidi kabisa haitakuwa rahisi kwa sababu ilikuwa sio tabia yako kabla, lakini ukiamua na ukaweka kwenye matendo, lazima itakuwa tabia yako.
 
Uvumilivu ni uwezo wa kuendelea bila kukata tamaa pale unapopita katika kipindi kigumu. Uvumilvu ni kiungo muhimu sana katika mafanikio yetu, iwe ni mafanikio ya kiroho, mafanikio binafsi, mafanikio ya kiafya, mafanikio kibiashara n.k. Bila uvumilivu hatutaweza kuyafikia malengo yetu makubwa
 
Watu wengi wanapenda njia ya mkato (shotcut). Wanataka wafanye kitu leo, kesho wapate majibu. Hawataki kuweka juhudi na kuvumilia. Hii imekuwa moja ya sababu ya wengi kutofanikiwa. Kuna msemo wa kingereza unasema ‘ always shortcut is a wrong cut’ ukimaanisha siku zote njia ya mkato sio njia sahihi. Kama unataka kufanikiwa juhudi na uvumilivu ni lazima.
 
Safari yetu ya mafanikio imejaa vipindi vingi vugumu. Watu wengi wanaopita katika vipindi hivi vigumu uwa wanakosa uvumilivu. Kuna changamoto/ majaribu/ magumu utayapitia katika safari yako ya mafanikio. Na magumu haya yanahitaji uvumilivu, uku ukiwa na imani kwamba ipo siku yataisha. Usipokuwa mvumilivu katika kipindi hiki kigumu ni lazima ukate tamaa.
 
Ufanye nini

Elewa uvumilivu ni tabia
Mafanikio hayana shotcut bila kuvumilia na kuweka juhudi
Kama umekosa uvumilivu kwenye mafanikio yako hasa kipindi unapopita katika magumu, ni wakati sasa wa kutengeneza tabia hii katika maisha yako.
Kumbuka tabia kama haikuwa yako inachukua muda mpaka iwe tabia yako.
 
Back
Top Bottom