Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji23][emoji23]shemeji bhana...
Halafu huwezi amini nilikuwa naitafuta kwa gallery yangu siioni,asante acha niirudishe kwa heshima yako[emoji4][emoji4][emoji4]
Asante sana shemeji kwa kuirudisha hii avatar. Huyu ndiye Carba orijino wengine wote feki. Hata Cole huko aliko bila shaka ni full magego. Thaaaaaaaaaaaanks.......
 
Kuna watu wanaoweka malengo na mipango ya maisha yao na kuna wale wasio na malengo na mipango ya maisha yao. Rafiki naamini una malengo na mipango ya maisha yako. Malengo na mipango hii unaweza ukawa umeiweka kichwani au umeaandika. Nakushauri kama unayo kichwani tu, basi chukua kalamu na uandike kwenye notebook yako. Hii itakusaidia kuwa na kumbukumbu nzuri.
 
Unakuta tuna mpango kwamba ikifika siku fulani tutafanya kitu fulani. Unakuta tuna malengo na mipango ya kufanya kwa baadae. Maneno kama ‘ikifika kesho nitafanya hiki na hiki’, ‘ kwa baadae nataka kuwa hivi na hivi’, ‘ kwa baadae nataka nipate hiki na hiki’ na mengine kama hayo, tumezoea sana kuyasema. Yote haya yanaonyesha kwamba tuna mpango na kesho yetu.
 
Mara nyingi tunapopanga mipango yetu tunaiweka kesho mbele kuliko leo. Kesho inakuwa na maana sana kuliko leo. Tunapanga kesho tutafanya nini na mara kadhaa kesho ikifika tunapeleka mbele tena, tunasema kesho, kesho inakuwa kesho, ukija kushituka miaka imepita bila kufanya chochote.
 
Mafanikio ni sasa sio kesho. Mtu anaweza akaangalia leo unafanya nini na akatabiri kesho utakuwa wapi. Kama ni afya yako, mtu anaweza akaona unavyokula au unavyotunza mwili wako, akajua kesho utakuwa wapi. Unaweza ukawa na mpango wa kuanza kula chakula bora mpaka upate kiasi fulani cha fedha. Rafiki mafanikio ni leo. Unatumiaje kiasi cha fedha ulichonacho kula chakula bora kwa ajili ya afya yako sasa.
 
1507392664182.jpg
 
Back
Top Bottom