Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

watu wengi wanakata tamaa wanapo ona mambo ni magumu. Watu wengi wanapokutana na changamoto wanashindwa kuendelea mbele. Matatizo yanapokuja, inakuwa ngumu sana kwao kuendelea mbele na safari yao ya mafanikio.
 
Ukweli ni kwamba mafanikio yamejaa mabonde na milima, hakuna tambalale kama wengi wanavyozani. Ukitaka kufikia ndoto zako, lazima ujue haitakuwa rahisi kuzifikia bila kukutana na magumu au changamoto.
 
Kama una uwakika na jambo unalofanya litakufikisha kwenye kitu unachotaka au ndio dhumuni lako, kuna mambo mawili ambayo unatakiwa kuyajua ili magumu au changamoto zinapokuja, uweze kuendelea mbele.
 
Unapoyaelewa mambo haya mawili na ukayaweka kwenye matendo, ni imani yangu utafika unakotaka kufika. Inewezekana kabisa isiwe rahisi lakini inawezekana kama ukiweka dhamira ya kweli na juhudi. Haya hapa ni mambo mawili (2) unayotakiwa kuwa nayo ili usikate tamaa unapokutana na magumu au changamoto;
 
Jambo la kwanza; Uvumilivu

Moja ya kitu kinachowafanya watu wengi kukata tmaa ni kutokuwa wavumilivu. Mambo yanapokuwa magumu watu wanashindwa kuvumilia. Kiukweli hakuna kitu rahisi rafiki yangu, lazima kuna maumivu utayapata kwenye safari yako ya mafanikio.
 
Ukishindwa kuvimilia maumivu, lazima utakata tmaa. Chochote unachotaka kubadili kwenye maisha yako lazima ukubali maumivu. Kutoka hapo ulipo kwenda unakotaka, sio rahisi, lazima uumie. Kama unakwepa maumivu, huwezi kufika unakotaka kufika.
 
Jifunze kuvumilia rafiki yangu, acha kukwepa maumivu. Hakuna mazuri bila kutoka jasho. Tafuta njia ya kuondokana na matatizo au changamoto unazokutaka nazo, lakini kumbuka bila uvumilivu hutafika popote. Hakuna kitu kizuri kinachokuja kwa ghafula, bila kuweka juhudi, kujituma na kuvumilia.
 
Jambo la pili; Muda

Moja ya kitu watu wengi wanakosea ni kutaka mafanikio ndani ya muda mfupi. Watu wanataka mambo yaende harakaharaka, wanataka waanze kuona majibu ndani ya muda mfupi. Rafiki hakuna mafanikio ya kudumu yanayopatikana ndani ya muda mfupi. Inaweza ikakuchukua miaka mitano mpaka kumi kupata hicho unachotaka. Wewe hata mwaka mmoja ujafikisha ushakata tamaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…