Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mawimbi kwenye mfumo wa fahamu husafiri kwa kasi ya mita 120 kwa saa (kilometa 200 kwa saa)

Inaelezwa kuwa unapomgusa mtu au kitu kinapomgusa mtu, tarifa za tendo hilo husafiri kwa kasi kubwa ya mita 120 kwa saa (kilometa 200 kwa saa) kuelekea kwenye ubongo.
 
Ubongo unaweza kutunza kiasi kikubwa cha kumbukumbu.

Kwa kipindi cha maisha ya binadamu yote, ubongo wake unaweza kutunza biti za data zipatazo milioni bilioni moja. Milioni bilioni moja? Ndiyo, milioni bilioni moja na zaidi.
 
Moyo unaweza kuendelea kudunda hata ukiwa nje ya mwili

Nini? Ndiyo, moyo unaweza kuendelea kudunda hata ukiwa nje ya mwili ikiwa tu utapata oksijeni. Moyo umeumbwa kwa namna ambayo unazalisha mawimbi yake ya umeme wenyewe yanayowezesha misuli yake kusukuma damu. Hii ndiyo sababu wataalamu wa tiba wanaweza kuutoa moyo na kuurudisha tena bila shida.
 
Naamini umejifunza mengi na kufurahia makala hii. Ni wazi kuwa kuna mambo mengi yakushangaza kuhusu miili yetu ambayo singeweza kuyaeleza yote hapa. Lakini naamini kwa mwanzo huu utapata hamasa ya kufanya utafiti zaidi juu ya mengine mengi.
 
Maziwa hufanya mambo mengi mazuri kwa ajili ya afya yako. Wataalamu wa afya na wauzaji wa maziwa wamekuwa wakieleza faida kadha wa kadha za kunywa maziwa. Je umewahi kujiuliza hasa ni faida gani hizo zitokanazo na unywaji wa maziwa?
 
Hujenga na kulainisha ngozi

Je unamfahamu Cleopatra? Cleopatra alikuwa ni malikia wa Misri anaesadikiwa kuwa mzuri sana. Inaaminikia uzuri wa Cleopatra ulitokana na tabia yake ya kuogea maziwa mara kwa mara.

Hivyo basi, ni wazi kuwa, vitamini na virutubisho vilivyoko katika maziwa ni muhimu kwa ajili ya ngozi bora. Ni vyema kunywa angalau bilauri moja ya maziwa kila siku.
 
Huimarisha meno

Maziwa ni chanzo bora cha madini ya kalisiamu, hivyo basi maziwa ndicho kitu halisi kinachohitajiwa na meno yetu. Pia maziwa huzuia kutoboka na kuoza kwa meno. Kalisiamu hufyonzwa na miili yetu kukiwa na vitamini D; hivyo jitahidi kunywa maziwa kwani maziwa huwa na vitamini D.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…