Kocha wa Yanga, George Lwandamina atamkosa mshambuliaji wake hatari raia wa Zimbabwe Donald Ngoma, baada ya taarifa ya daktari wa timu hiyo kuthibitisha ukubwa wa tatizo alilokuwa nalo.
Lwandamina ameiambia Goal, kumkosa Ngoma ni pengo kubwa katika safu yake ya ushambuliaji hasa katika mechi ngumu inayowakabili Jumamosi hii dhidi ya Kagera Sugar.