Messi alikuwa wa pili baada ya Ronaldo katika kura za msimu uliopita, Antoine Griezmann akishika nafasi ya tatu.
Nyota wa paris Saint-Germain Neymar alishika nafasi ya nne katika tuzo za FIFA 2016, lakini amepanda tatu bora mwaka huu sambamba na mchezaji mwenzake wa zamani wa Barcelona Messi.
Kulikuwa na wachezaji 24 katika orodha ya awali, Gianluigi Buffon, Paulo Dybala, Griezmann, Harry Kane, Sergio Ramos na Alexis Sanchez miongoni mwa majina yaliyokatwa kabla ya kupatikana matatu a mwisho.