Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mwili unahitaji chakula chenye mchanganyiko wa makundi haya ya chakula ili kuwa na afya bora na iliyo imara kama inavyolinganishwa na nyumba imara. Inajulikana kuwa mchanga ukizidi katika tofali nyumba itamomonyoka nakuanguka au cementi ikipungua pia nyumba itamomonyoka na kuanguka. Hii ni sawa na ulaji kwa binadamu, chakula kikiwa hakina au kina kiwango kidogo cha baadhi ya makundi ya chakula yaliyotajwa hapo juu lazima mwili utakuwa dhoofu, hata makuzi yake hayatakuwa mazuri. Magonjwa yatokanayo na utapiamlo ndio chanzo kikuu cha mwili kuwa na afya mbaya. utapia mlo hutokana na lishe duni au lishe iliyozidi.
 
Lishe duni ni hali ya mwili kukosa baadhi ya virutubishi vinavyohitajika mwilini, kama vile protini, wanga, mafuta, vitamini na madini. Mwili ukikosa baadhi ya virutubishi hivi hushindwa kufanya kazi zake za kimebotali vizuri na kusababisha madhara mengine mengi. Vilevile mwili ukiwa na lishe iliyozidi husababisha madhara makubwa hii inatokana na kubadilika kwa baadhi ya kazi za seli na ogani mbalimbali mwilini.
 
Magonjwa ya utapia mlo ni kama vile: kwashakoo, marasmasi, marasmasi na kwashakoo, upungufu wa damu (Iron Deficiency Anaemia), tatizo la ukosefu wa vitamini C, tatizo la Ukosefu wa vitamini A, tatizo la ukosefu wa madini Joto, na magonjwa yatokanayo na lishe iliyozidi ni kama kisukari, presha, magonjwa ya moyo ambayo ndio tatizo kubwa linalowakumba hasa matajiri wanaojikita zaidi katika vyakula vyenye mafuta mengi na sukari.
 
Vyakula vya aina ya mikunde na vyenye asili ya wanyama
  • Maharage, kunde, mbaazi, soya, karanga,njegere, njugu mawe,dengu, choroko, asili ya wanyama ni: nyama, mayai, samaki, dagaa, kumbikumbi, senene, maziwa na nzige.
Virutubishi: Protini
  • Hujenga mwili. Huwezesha mwili kutengeneza seli nyingine.
 
Mboga-mboga
  • mchicha, majani ya kunde, majani ya maboga, kisamvu, matembele, spinachi, mgagani, mlenda, mnavu, mchunga, karoti, pilipili hoho, nyanya chungu, biringanya, bamia, kabichi, figiri, sukuma wiki na chainizi.
Virutubishi: Vitamini na Madini
  • Huupa mwili kinga imara dhidi ya maradhi mbalimbali.
 
.Matunda
  • mapera, maembe, machungwa, papai, nanasi, zambarau, dhabibu, mapesheni, machenza, ubuyu, ukwaju, limao
Virutubishi: vitamini na madini
  • Huupa mwili kinga dhidi ya maradhi.
  • Husaidia kwa baadhi ya virutubishi kutumika kwa ufasaha zaidi mwilini.
 
Mafuta na Sukari
  • mafuta ya kupikia, ufuta, karanga, mbegu za alizeti, siagi, samli, nyama yenye mafuta, sukari ni: asali, miwa, vyakula vinavyotengenezwa kwa sukari nyingi kama jamu, keki, n.k
virutubishi: mafuta
  • Huupa mwili nguvu.
  • Husaidia ufyonzwaji wa vitamini A,D,E na K.
 
78e0fb.jpg
 
Maji hayakuwekwa kwenye kundi lolote la chakula kwa sababu hayana virutubishi. Ni muhimu kunywa maji safi na salama kwani yanarahisisha umeng'enyaji wa chakula, kusafirisha virutubishi na kutoa uchafu ambao hutengenezwa mwilini wakati mwili unafanya kazi zake. Asilimia kubwa ya mwili ni maji hivyo ni vyema kunywa maji mara kwa mara ili kuwa na afya bora.
 
Utapia mlo ni hali ya kuwa na lishe duni au iliyozidi ambayo huambatana na matatizo mbalimbali ya kiafya. ni hali inayotokana na kula chakula chenye virutubishi visivyotosheleza au virutubishi vilivyozidi kana kwamba kinasababisha matatizo ya kiafya. ulaji wa vyakula vyenye virutubishi kidogo au pungufu hutokana na ulaji usiohusisha makundi matano ya vyakula, kwa mfano watanzania wengi hula vyakula vya aina moja kwa mida tofauti, mfano zaidi: asubuhi labda amekunywa uji, mchana akala ugali,makande au wali, jioni akala ugali au pilau. hii inaonyesha kuwa mlaji amekula chakula kilekile kwa kubadili mapishi tu, yaani badala ya uji akala ugali au makande, badala ya wali akala pilau, hapa atakuwa amekula virutubishi vya aina moja mara kwa mara. ulaji huu husababisha mwili kukosa baadhi ya virutubishi na kupelekea magonjwa na matatizo ya utapiamlo.
 
SIMULIZI YA MFALME MTATA NA MCHAMUNGU. Baada ya salaam na mazungumzo mafupi Mchamungu akafunguka. "Bwa mfalme nimekuja kwako kwakuwa nimepatwa na mtihani, mtihani wangu hasa unahitaji fedha, baada ya kutafakari kwa kina nikaona nije kwako maana uwezo wa kunikopesha au kunisaidia unao, hata hivyo ikitokea kwamba nawe huna ninachohitaji, hakuna shida, hivyo sina kinyongo. Maana naamini mwenyezi mungu aliyenipa mtihani, pia ana uwezo kuniondolea mtihani huu kwa jinsi anavyoona inafaa". Mfalme akajibu, "Mchamungu una shida, halafu unajifanya mungu atatatua shida zako, mimi ningeweza kukupatia hicho unachotaka, lakini hata nikikupa utajifanya ni uwezo mungu wako. kwakifupi nenda ukaseme na mungu wako umalize shida zako kwa jinsi unavyojua mwenyewe". Mchamungu akajibu, hata hilo pia nashukuru maana Mungu ninayemuamini hashindwi kutatua changamoto nilizonazo, maana ana nguvu na uwezo. kwamba aweza kukufanya dhalili hata wewe mfalme mwenye nguvu, akakushusha. Kauli hii ilizidi kumkera Mfalme. akasema. Ufalme huu nimerithi kwa vizazi na vizazi nyuma, kufikiria Mungu anishushe kwa kupoteza cheo nilichonacho na mali nilizonazo ni ndoto zako tu bw Mchamungu" Kwahiyo naomba uondoke. Mchamungu akaenda zake
 
Vilevile ulaji unaozidi kiwango husababisha virutubishi kuzidi mwilini na kujikusanya katika sehemu mbalimbali za mwili. kujikusanya kwa virutubishi hivi huweza kubadili kazi za seli au mifumo mbalimbali ya mwili. ulaji wa vyakula vya mafuta mengi na sukari au vyakula vinavyopikwa kwa mafuta mengi ndio chanzo kikubwa cha mtu kuwa na mkusanyiko wa mafuta mwilini na kuwa na uzito uliozidi. vyakula kama chipsi, nyama choma, soda, vyakula vinavyopikwa kwa mda mfupi (fast foods), sukari, biskuiti, jam, keki, n.k.
 
Back
Top Bottom