Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Dalili:
-unyafuzi uliozidi
-ngozi hukauka
-baadhi ya sehemu za mwili husinyaa na kuning'inia (matako, korodani, kwapa)
-ngozi huvutika sana (tishu za ngozi huwa hazina mafuta)
-huonekana amekonda sana.
-anahamu kubwa ya kula.
-uso huwa kama wa nyani/mdogo
-macho yao huwa makubwa
-tumbo lao huwa limevimba
-hulia mara kwa mara
-ngozi imekauka/sinyaa
-nyuso zao ni nyembamba/ndogo.
 
713_jlo.jpg
 
Dalili:
-unyafuzi uliozidi
-ngozi hukauka
-baadhi ya sehemu za mwili husinyaa na kuning'inia (matako, korodani, kwapa)
-ngozi huvutika sana (tishu za ngozi huwa hazina mafuta)
-huonekana amekonda sana.
-anahamu kubwa ya kula.
-uso huwa kama wa nyani/mdogo
-macho yao huwa makubwa
-tumbo lao huwa limevimba
-hulia mara kwa mara
-ngozi imekauka/sinyaa
-nyuso zao ni nyembamba/ndogo.
 
Marasmasi na kwashakoo.
Ugonjwa huu hutokana na ukosefu wa viini vya protini na wanga mwilini kwa pamoja. Yaani kutokula chakula chenye makundi ya chakula ambayo kundi la kwanza ni vyakula vyenye jamii ya kunde na vyenye asili ya wanyama, na la pili ni vyakula vya Nafaka, Mizizi na Ndizi. Pia ugonjwa huu mara nyingi huwapata watoto.
 
Tatizo la Ukosefu wa vitamini A. (ukavu macho)
tatizo hili husababishwa na kutokula chakula chenye vitamini A kama vile mbogamboga na matunda, inajulikana kuwa matunda na mbogamboga zenye rangi ya njano/machungwa vina vitamini A kwa wingi zaidi. viazi vya njano (viazi lishe), na karoti zina vitamini A nyingi zaidi. mbogamboga zingine pamoja na matunda pia yana vitamini A nyingi. Vitamini A hufonzwa kwa ufasaha zaidi chakula kikiwa na mafuta kias
 
Tatizo la Ukosefu wa Madini Chuma (Iron Deficiency Anaemia)
Tatizo hili huwapata sana watoto na wanawake, pia watu katika makundi mengine hupatwa na tatizo hili. Tatizo hili husababishwa na kutokula chakula chenye viini vya madini ya chuma kama vile mbogamboga, nyama, mayai, juisi ya rosella, n.k, pia utumiaji wa vidonge vya madini ya chuma kama inavyoshauriwa na dakitari huongeza damu. malaria na minyoo husababisha upungufu wa damu pia. madini chuma hufonzwa kwa ufasaha panapokuwepo na chakula chenye vitamini C kama ubuyu, ukwaju, machungwa, limao, n.k. hivyo ni vema kula vyakula vyenye madini chuma pamoja na vyenye vitamini C ili kuwezesha ufyonzwaji wa madini chuma kwa ufasaha zaidi. Epuka vizuizi vya madini chuma katika ufyonzwaji wake kama vile kahawa, chai, ugoro, tumbaku, na vinywaji vya cocacola kwa saa moja kabla au baada ya kula chakula chenye madini chuma. zuia ugonjwa wa malaria kwa kulala kwenye chandarua, kutibu malaria haraka baada ya kuugua, pata vidonge vya kujikinga na malaria (SP) hasa wajawazito. jikinge na minyoo kwa kuvaa viatu, meza vidonge vya minyoo mara mbili kwa mwaka, tumia vyoo kujisaidia haja kubwa na ndogo na osha mikono kabla na baada ya kula.
 
Tatizo la Ukosefu wa Madini Joto (Iodine Deficiency Disorder)
Tatizo hili husababishwa na kutokula chakula chenye madini Joto. madini joto hupatikana kwenye chumvi yenye madini joto (iodized salt), hasa chumvi hii hupatikana madukani. Ugonjwa ujulikanao kama Goita ndio husababishwa na ukosefu wa madini Joto.
 
Back
Top Bottom