Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

SIMULIZI YA MFALME NA MCHAMUNGU. Siku chache baadaye, Mfalme akamchagua Farasi wake aliye bora na mzuri kuliko wote, akiwa na jopo lake la walinzi na wapambe akaingia mtaani akitembea tembea kufurahia nchi yake. Katika pitapita yake wakojikuta wapo sokoni, mbele yao kundi kubwa la watu limuzunguka wakishangaa kitu. Mfalme akauliza "pale pana nini"? Akaambiwa kuna mtu toka kusikojulikana amekuja na farasi mzuri ajabu, ni farasi wa kushangaza ambaye utatamani kumtazama. "Yani bwana mfalme hata wewe na ufalme wako wote hujawahi na hutawahi kumiliki farasi kama huyo". Mfalme akafura kwa hasira, kwamba kwenye nchi yangu raia tu amiliki kitu kizuri kuliko mimi Mfalme!!? Akajisemea hii sasa ni dharau, lazima nilishughlikie vilivyo HAIWEZEKANI.
 
KISA CHA MFALME MTATA NA MCHAMUNGU. Mfalme na jopo lake akajisogeza mahali pale ili naye aone maajabu ya Farasi. Na kweli, Mfalme akamuona Farasi mweupe, mwenye afya, nzuri, amewekewa matandiko yenye uzuri wa kipekee, akiwa na vikuku vya ajabu kabisa. Mfalme akashikwa na donge rohoni[emoji3]. Hivyo Mfalme akamkabiri mgeni yule, akamuuliza anatoka wapi,akamwambia anapita njia toka nchi ya mbali, akiwa na safari zake za kuitembelea dunia. Kama ilivyo kawaida ya Wafalme na baadhi ya matajiri, huwa hawapendi kuzidiwa kwa mavazi, majengo, vyombo vya usafiri nk, akamuomba mgeni yule amuuzie Farasi huyo. Yule mgeni akajibu kuwa farasi hauzwi. Mfalme akafanya kampeni na ushawishi wa kila aina. yule mgeni akamwambia mfalme kuwa farasi yule hatamuweza, lakini Mfalme akawa hashikiki. Mwisho yule mgeni akamuuzia Farasi huyo. Mfalme alipolipa tu akamkalia farasi. Sekunde chache baada ya kumkalia Farasi akaruka kwa kasi ya umeme na kudondokea msituni mahali pasipojulikana akiwa na Mfalme mgongoni mwake. Fumba na kufumbua Mfalme akajikuta peke yake bila mlinzi wala mpambe akiwa na farasi tu kwenye msitu mnene na wa kutisha. Katika hali hiyo kushangaa shangaa na uoga wa mahali alipo, farasi akaruka tena, safari hii Mfalme alidondoshwa chini na farasi aliruka mwenyewe na kumuacha Mfalme msituni akishangaa shangaa ITAENDELEA....
 
Another MD in da house. Uzi huu safi sana !!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…