Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Screenshot_2017-10-12-15-01-32.png
 
Lisaa na Masaa

Lisaa na Masaa ni misamiati au maneno ambayo yamezoeleka sana hasa kutokana
na kutumiwa sana kwenye vyombo vya habari.

Mfano:

Hotuba ya raisi imetumia takriban lisaa limoja.

Michezo ya ligi kuu ilikuwa ya masaa mawili.

Sentensi hizo hapo juu siyo sahihi, kwani hakuna neno lisaa na masaa katika
Kiswahili sanifu. Badala yake sentensi hizi zilitakiwa ziwe kama ifuatavyo.

Hotuba ya raisi imetumia takriban saa moja.

Michezo ya ligi kuu ilikuwa ya saa mbili.
 
Nona na nenepa

Maneno mengine ambayo yanatumiwa kimakosa ni neno nona na nenepa.

Mfano:

Hamisi amenona sana siku hizi.

Ng’ombe wangu wamenenepa sana mwaka huu.

Katika sentensi hizi neno nona limetumika vibaya kwani kinachonona ni
mnyama na sio mtu. Vivyo hivyo kinachonenepa ni mtu na sio mnyama. Sentensi
sahihi zilitakiwa ziwe kama ifuatavyo:

Hamisi amenenepa sana siku hizi.

Ng’ombe wangu wamenona sana mwaka huu.
 
Jangili

Neno jangili hutumiwa vibaya na wazungumzaji wa lugha bila kuzingatia maana
yake halisi.

Mfano.

Majangili yamevamia hoteli huko Nairobi.

Maana halisi ya jangili ni mtu anayeuwa wanyama pori bila kibali au bila
kufuata sheria. Hivyo wanaovamia hoteli ni majambazi na si majangili kama
ilivyotumika katika sentensi hiyo hapo juu. Sentensi sahihi ingeweza kuwa:

Majambazi yamevamia hoteli huko Nairobi.
 
Kama unapenda kusikiliza mziki basi uko kwenye kundi zuri. Watu mbalimbali maarufu wamewahi kutoa maoni yao kuhusu mziki kama vile mwanabayolojia Charles Darwin aliyesema kuwa angepewa nafasi ya kushi tena angetengeneza kanuni ya kusoma mashairi na kusikiliza mziki angalau mara moja kwa wiki. Kwa upande mwingine Albert Einstein alikiri kuwa asingekuwa mwanafizikia basi angekuwa mwanamziki.
 
Mziki hutufanya tuwe na furaha

William James alsisema “Siimbi kwa sababu ninafuraha, bali nafurahi kwa kuwa ninaimba” .

Kusikiliza mziki huzalisha kemikali ya dopamane ambayo hutufanya tujisikie vizuri. Hii ndiyo sababu mtu akiwa anajisikia vibaya au kukosa furaha mara nyingi anaposikiliza mziki hasa wa taratibu hujisikia vizuri.
 
Huongeza ufanisi katika kukimbia

Mtafiti Marcelo Bigliassi na wenzake walibaini kuwa wakimbiaji wanaosikiliza mziki walimaliza mbio za mita 800 haraka zaidi kuliko wengine. Hivyo ni dhahiri kuwa kusikiliza mziki wakati wa kukimbia kunaweza kuwa kama hamasa zaidi. Unaweza kusikiliza mziki wa haraka haraka au taratibu kulingana na vile unavyopendelea.
 
Mziki huondoa msongo na kuboresha afya

Kusikiliza mziki hupunguza kwa asilimia 60 homoni zinazosababisha msongo (stress). Ikiwa basi msongo utapungua ni dhahiri kuwa pia maradhi mengi ambayo chanzo chake ni msongo yatapungua kama si kwisha kabisa. Unaweza kusikiliza mziki na kuimba wakati mziki unapoimba; pia usisahau kucheza angalau kwa kuchezesha mguu ili kupata tiba hii kamili.
 
Ulishawahi kujiuliza ni kwanini ukisikiliza mziki wa taratibu mara nyingi unapatwa na usingizi? Ni dhahiri kuwa mziki una nafasi kubwa katika kulala kwetu. Inashauriwa wakati wa usiku kuweka ubongo wako katika hali nzuri ili uweze kulala vyema; unaweza kusikiliza mziki wa taratibu kabla ya kulala.
 
Mziki hukuweka katika hali nzuri unapoendesha gari

Wakati mwingine kuendesha gari ni kazi inayochosha; hivyo inahitaji kiburudisho ili kuifanya vyema. Ni dhahiri kuwa madereva wanaoendesha magari masafa marefu hupenda kusikiliza mziki ili kujiweka katika hali (mood) nzuri. Hivyo baisi, unaweza kusikiliza mziki unapoendesha gari. Kumbuka kuzingatia sheria za barabarani; usisikilize kwa sauti kali kiasi cha kushindwa kusikia sauti nyingine barabarani kama vile honi ili kuepuka ajali.
 
Hukuwezesha kujifunza na kukumbuka

Baadhi ya watu wamebainisha kuwa wanaposoma au kujifunza mambo kadhaa wakati wakisikiliza mziki, basi hufanikiwa kuyamudu maswala hayo vyema. Si jambo la kustaajabisha kuwaona watu wakisikiliza mziki huku wakisoma vitabu, majarida, tovuti nk.
 
Hata hivyo, hili linategemea mtu na mtu, wengine hawapendi kusoma au kujifunza huku wakisikiliza mziki, wakati wengine hupenda kufanya hivyo. Hivyo uamuzi ni wako kuwa unapenda mziki au laa; na ni mziki wa namna gani unaopenda wakati wa kusoma na kujifunza.
 
Back
Top Bottom