Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wenger alithibitisha kuwa atazungumza na Alexis Sanchez kuelekea safari yao ya Watford baada ya nyota huyo kushuhudia Chile ikinyukwa 3-0 dhidi ya Brazili.
Arsena watasafiri kwenda Watford wakiwa hawajafungwa katika mechi saba kwenye michuano yote, wakati Hornets wakiwa hawajafungwa mechi mbili za ligi
 
1507834474462.jpg
 
Arsene Wenger amesema "inawezekana" Alexis Sanchez na Mesut Ozil wanaweza kuondoka Arsenal dirisha la uhamisho Januari.
Nyota hao wawili wapo kwenye mwaka wa mwisho wa mikataba yao Emirates klabu kadhaa za Ulaya zikifuatilia mwenendo wao.
Goal ilibainisha wiki iliyopita kuwa Alexis ameiweka wazi bodi ya Arsenal kuwa hana mpango wa kusaini mkataba mpya, Manchester City na Paris Saint-Germain zikiwa klabu zenye nafasi kubwa kuipata saini yake.
 
Ozil amezivutia Manchester United na Barcelona, lakini anataka kubaki London na wakala wake Erkut Sogut amebainisha Jumatano kuwa mazungumzo ya mkataba mpya na Arsenal yanaendelea vizuri.
Hata hivyo, Wenger amesema kuwa bado inawezekana wachezaji wote hao wawili kuondoka dirisha la majira ya baridi likifunguliwa.
 
Akiongea kuelekea mechi ya Ligi Kuu Uingereza Arsenal dhidi ya Watford itakayopigwa Jumamosi, alisema: "Katika hali yetu tumeshafikiria suluhisho kwa hali zote. Inawezekana."
Alipoulizwa hasa kuhusu mustakabali wa Ozil katika klabu, Mfaransa huyo alijibu: "Namuelewa [kwamba anataka kubaki].
"Nadhani hali inaweza kugeuka. Kwa sasa, hatupo karibu kutangaza chochote."
 
Wenger alithibitisha kuwa atazungumza na Alexis Sanchez kuelekea safari yao ya Watford baada ya nyota huyo kushuhudia Chile ikinyukwa 3-0 dhidi ya Brazili.
Arsena watasafiri kwenda Watford wakiwa hawajafungwa katika mechi saba kwenye michuano yote, wakati Hornets wakiwa hawajafungwa mechi mbili za ligi.
 
Kocha Ettiene Ndayiragije, kesho atakuwa na kibarua kigumu cha kuikabili timu ya Mbeya City, inayofundishwa na kocha raia mwenzake wa Burundi Nsanzurwimo Ramadhani katika mchezo wa mzunguko wa sita wa ligi kuu ya Tanzania Bara.
Pambano hilo litapigwa uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza nyumbani kwa Mbao FC, na timu hiyo inapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo dhidi ya wageni wao Mbeya City ambao hawana mwanzo mzuri msimu huu.
 
Huo utakuwa ni mchezo wa tatu kwa Mbao kucheza nyumbani na watalazimika kushinda ili kuandikisha ushindi wa kwanza kwasababu katika mechi mbili walizocheza kwenye uwanja huo msimu huu wamepata sare matokeo ambayo wayewaweka kwenye nafasi za chini kwenye msimamo.
Pamoja na kuwakosa wachezaji wenye majina makubwa lakini Mbao imeonekana bado n timu imara ambayo inaweza kucheza na kupata matoke bila kujali inacheza na timu ya aina gani kitu ambacho kinafanya wapewe nafasi ya kushinda.
 
Uwepo wa nahodha Boniface Maganga,Habibu Haji na nahodha wao Yusufu Ndikumana, unampa matumaini kocha Ndayiragije, ambaye tumaini lake kubwa ni kuiona Mbao inafanya maajabu msimu huu kwa kutwaa ubingwa wa Tanzania na kushiriki michuano ya kimataifa mwakani.
Ndayiragije amesema mchezo wa kesho ni mgumu, kwasababu Mbeya City, ni timu nzuri na inawachezaji wazuri wenye uzoefu lakini watapambana kuhakikisha wanshinda mchezo huo wa nyumbani.
 
Nmafahamu vizuri kocha Ramadhani wa Mbao, ni kocha mzuri na tuna fahamiana lakini kupitia mchezo huo nataka kumkaribisha Tanzania, na kumweleza ushindani uliopo kwenye ligi hii ambayo ni ngumu kwa kiasi fulani,”amesema Ndayiragije.
Kocha huyo amesema katika mchezo wa kesho kikosi chake hakitakuwa na mabadiliko makubwa na mfumo atakaoutumia ni ule wa 4-3-3 , ambao utamsaidia kukaba na kushambulia akiwa na washambuliaji wengi.
 
Kwaupnde wake kocha msaidizi wa Mbeya City Mohamed Kijuso, ameseam wamekwenda Jijini Mwanza wakifahamu kuwa Mbao ni timu bora na ngumu, na wahaiheshimu lakini anajivunia maandalizi mazuri waliyonayo chini ya kocha mpya Ramadhani.
Kijuso amesema wachezaji wao wote wenye waliowasajili wamekwenda nao Mwanza na wamefanya hivyo kwasababu wamepania kushinda mchezo huo ili kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi.
 
Kwaupnde wake kocha msaidizi wa Mbeya City Mohamed Kijuso, ameseam wamekwenda Jijini Mwanza wakifahamu kuwa Mbao ni timu bora na ngumu, na wahaiheshimu lakini anajivunia maandalizi mazuri waliyonayo chini ya kocha mpya Ramadhani.
Kijuso amesema wachezaji wao wote wenye waliowasajili wamekwenda nao Mwanza na wamefanya hivyo kwasababu wamepania kushinda mchezo huo ili kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi.
 
Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Free State ya Afrika Kusini, na wengine ni miongoni mwa nyota wenye majina makubwa waliosafiri na kikosi cha Mbeya City, kwa ajili ya pambano hilo ambalo linatarajiwa kufanya maajabu kwa kuifunga Mbao.
Hiyo itakuwa ni mechi ya kwanza Mbeya City, kucheza chini ya kocha mpya Ramadhani, baada ya uongozi wa timu hiyo kumtimua kazi aliyekuwa kocha wake mkuu raia wa Malawi Kinnah Phir, kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo.
 
Katika mchezo huo wa kesho Kijuso amesema mfumo ambao wamepanga kuanza nao ni ule wa 4-4-2, na hiyo ni kutokana na wachezaji wao wengi kuufahamu vizuri na ndiyo uliowasaidia kupata matokeo kwenye baadhi ya mechi zao.
 
Kikosi cha Yanga kinatarajia kuondoka jioni ya leo kwa mafungu kuelekea Bukoba ambapo Jumamosi wataikabili Kagera Sugar, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, utakaopigwa uwanja wa Kaitaba.
Meneja wa Yanga Hafidhi Salehe, ameiambia Goal, kundi la kwanza litaondoka saa 10, jioni ya leo na litakwenda kulala Mwanza kabla ya kesho kuunganisha na ndege kwenda bukoba na kundi la pili litaondoka Dar es Salaam kesho alfajiri likielekea moja kwa moja Bukoba.
 
Sababu ya kushindwa kuondoka kwa pamoja ni kutokana na kukosa ndege ya pamoja, lakini hiyo siyo mbaya kwasababu kitu cha msingi ni kufika kituoni Bukoba, na limewezekana kilichobaki ni kuhakikisha tunacheza na kupata ushindi kwenye mchezo huo,”alisema Salehe.
Kiongozi huyo amesema wanakwenda Bukoba, bila ya mshambuliaji wao Donald Ngoma aliyeumia nyama za baja kwenye mchezo uliopita dhidi yaMtibwa Sugar, lakini pia bado kuna wasiwasi ya kumkosa kiungo Mzimbabwe Thabani Kamusoko, ambaye leo asubuhi alionekana akifanya mazoezi ya peke yake.
 
Meneja huyo amesema kitu kizuri kwao ni kurejea kundini kwa mshambuliaji wao tegemeo Amissi Tambwe, ambaye atakuwepo kwenye msafara huo wa kikosi cha Yanga ambacho kinashika nafasi ya sita kwneye msimamo baada ya kucheza mechi tano na kushinda mbili huku ikienda sare mechi tatu.
Mbali ya kumkosa Ngoma wachezaji wengine ambao watakosekana kwenye kikosi cha Yanga ni kipa namba tatu Ramadhani Kabwili na kiungo mshambuliaji chipukizi Said Mussa ambao wapo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes’.
 
Back
Top Bottom