Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Screenshot_2017-10-14-13-11-20.png
 
Sababu kuu za magoli ya United ni Romelu Lukaku, ambaye amecheka na nyavu mara 11 katika mechi 10 kwenye michuano yote tangu atue Old Traffod
Manchester United wanaweza kukwea kileleni jedwali la Ligi Kuu ikiwa watashinda katika mechi yao ya Jumamosi wikiendi hii, lakini pia watalazimika kuwadhibiti vema mahasimu wao Liveprool katika uwanja wa Anfield.
 
Mashetani Wekundu wameanza kampeni za 2017-18 kwa kiwango cha hili ya juu wakijikusanyia pointi 19 kati ya 21, kadhalika magoli 21 katika wastani wa matatu kwa mechi.
Moja ya sababu kuu za magoli hayo mbele ya goli ni Romelu Lukaku, ambaye amecheka na nyavu mara 11 katika mechi 10 kwenye michuano yote tangu atue Old Trafford akitokea Everton.
 
Goli jingine katika uwanja wa Anfield litamfanya Mbelgiji huyo kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya Manchester United kufunga katika mechi nane kati ya nane za kwanza kwenye Ligi Kuu kwa klabu hiyo, lakini ana rekodi gani dhidi ya Liverpool?
 
Mechi ya kwanza kwa Lukaku dhidi ya Liverpool ilikuwa kipindi anaichezea Chelsea msimu wa 2011-12, akitokea benchi kuchukua nafasi ya Daniel Sturridge zikiwa zimebaki dakika 20.
Wakati anaingia, Chelsea tayari walikuwa wameshachapwa 4-1 Anfield na Lukaku alishindwa kuleta mabadiliko katika mechi hiyo. Mbelgiji huyo alipewa nafasi ya kuanza kwenye mechi ya Kombe la EFL robo fainali kwenye uwanja wa Stamford Bridge mwaka huo ambako Liverpool walishinda 2-0.
 
Lukaku alifurahia mafaniko mazuri akicheza kwa mkopo West Bromwich Albion, na mafanikio yake yaliendelea akiikabili Liverpool mara mbili katika kampeni ya Ligi ya Uingereza 2012-13.
Baggies walishinda mechi zote - 3-0 nyumbani na 2-0 katika uwanja wa Anfield - Lukaku akifunga goli la mwisho katika kila moja licha ya kuanzia benchi kwa mechi zote. Hata hivyo alikuwa miongoni mwa timu iliyofungwa kwenye raundi ya tatu Kombe la EFL msimu huo pia.
 
Back
Top Bottom