Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mafanikio binafsi ya Lukaku dhidi ya Liverpool yaliendelea kidogo akiwa Everton, Mbelgiji huyo akifunga mara mbili kwenye mechi yake ya kwanza ya ligi dhidi ya Reds katika sare ya 3-3 kwenye uwanja wa Goodison Park Novemba 2013.
Hata hivyo, Lukaku hakuweza kushinda katika mechi zake kubwa nane za Merseyside dhidi ya Liverpool akiwa na Tofees na amefunga mara moja tu katika mechi saba dhidi ya Reds.
Goli hilo lilipatikana Goodison Park Oktoba 2015, Lukaku akifunga goli lake kipindi cha kwanza dhidi ya Liverpool kusawazisha bao la Danny Ings.
 
Screenshot_2017-10-14-13-12-01.png
 
Antonio Conte amekiri kuzungumza na Charly Musonda kuhusu tabia ya tofauti aliyoonyesha na kumtaka kufanya jitihada dimbani kuliko mtandaoni
Kocha mkuu wa Chelsea Antonio Conte amesema kuwa hana shida na Charly Musonda baada ya kinda huyo kufunguka kuwa hakufurahia kukosa nafasi za kucheza Stamford Bridge.
 
Musonda alitumia mitandao ya kijamii kutoa maoni yake juu ya swala hilo, ripoti zikidai kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 atatolewa kwa mkopo dirisha la uhamisho Januari.
Hata hivyo, Conte amekiri kuongea na Musonda, Muitaliano huyo alidokeza kuwa anaangalia mbele na anamtaka mchezaji huyo kuweka nguvu nyingi kwenye maendeleo yake.
 
Conte, 48, aliwaambia wanahabari: "Nimeongea naye na nadhani Charly anatambua kosa lake. Kwa kweli nadhani anahitaji kuendelea kujitahidi sana kujiimarisha na hasa kifiziki. Akili yake inapaswa kuwa dimbani, siyo kwenye mitandao ya kijamii. Nimemwambia hili.
"Jukumu langu ni kumsaidia kupita njia sahihi, si njio ya upotevu. Zaidi ya yote unapokuwa na wachezaji wadogo ni muhimu kuzungumza naye, kuwaeleza namna ya kuchagua njia sahihi. Nimefanya hili na naamini ameelewa. Sioni tatizo lolote kwake.
 
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amedai kuwa anafurahia fursa ya kucheza dhidi ya Liverpool katika uwanja wa Anfield
Mourinho ataondoka na United kwenda Merseyside Jumamosi kwa mechi ya kwanza dhidi ya wapinzani wakubwa katika mbio za taji Ligi ya Uingereza, United wakitaka kuendeleza mwendo mzuri wa ushindi.
 
Mourinho aliwaambia waandishi: "Watu wanapozungumzia angahewa ni kama vile hatuipendi. Ndicho tunachotaka. Nashangaa mnapolizungumzia jambo hili katika mtazamo hasi. Nashangazwa zaidi wachezaji wa zamani wanapozungumzia angahewa kana kwamba ni jambo la kuhofia. Kama tungekuwa na hali inayofanana katika kila mechi basi ningekuwa na hofu.
 
Barca walipocheza dhidi ya Las Palmas katika uwanja mtupu, walikuwa wanafurahia hilo? Je! Las Palmas wasingependa kucheza Nou Camp pakiwa pamejaa? Tunapocheza nyumbani tunalalamika kukiwa hakuna ushabiki wa ukweli. Tunatambua kwamba wachezaji ni watu wenye uhasama. Ndicho tunachotaka. Tunafurahia kupata fursa nyingine kucheza katika hali hii. Inapendeza kucheza Anfield."
 
Mchezaji Nemanja Matic amedai Manchester United watakuwa makini kwa dakika 90 zote wakati dhidi ya Liverpool huko Anfield siku ya Jumamosi.
Manchester United wameshinda mechi sita katika michezo saba ya Ligi Kuu, wakati katika Ligi ya Mabingwa wamefanikiwa kushinda michezo yote miwili.
 
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 aliiambia MUTV: "Tumejitayarisha vizuri, meneja alipata video kwa ajili yetu kuona ni nini (Liverpool) walichonacho na jinsi tunaweza kuwazuia, kwa hiyo nina hakika tutakuwa tayari kuwadhibiti wao.
"Ni kama kila mchezo - tunapaswa kuzingatia kwa dakika zote 90, tunapaswa kuwa makini na vitu vidogo vidogoi, kwa sababu yanaweza kuwa hatari.
 
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 aliiambia MUTV: "Tumejitayarisha vizuri, meneja alipata video kwa ajili yetu kuona ni nini (Liverpool) walichonacho na jinsi tunaweza kuwazuia, kwa hiyo nina hakika tutakuwa tayari kuwadhibiti wao.
"Ni kama kila mchezo - tunapaswa kuzingatia kwa dakika zote 90, tunapaswa kuwa makini na vitu vidogo vidogoi, kwa sababu yanaweza kuwa hatari.
 
Back
Top Bottom