Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Screenshot_2017-10-14-13-35-02.png
 
Kocha George Lwandamina, atamkosa mshambuliaji Donald Ngoma, lakini atakuwa anafurahia kurejea kwa mshambuliaji Amissi Tambwe pamoja na kiungo Papy Kabamba Tshishimbi, ambaye alikosa mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, wiki moja iliyopita.
Yanga inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 6-2, katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa msimu uliopita ambapo timu hiyo ilikuwa chini ya kocha Mdachi Hans van der Pluijm, anayeifundisha Singida United hivisasa.
 
Mabingwa hao watetezi wamekwenda Kagera, lakini wanaonekana kutokuwa fiti ipasavyo kutokana na mwenendo mbaya walioanza nao msimu huu na kuwafanya hadi sasa kushika nafasi ya sita wakiwa na pointi 9.
Tegemezi kubwa la Yanga, tangu kuanza kwa msimu huu ni mshambuliaji Ibrahim Ajibu , ambaye amesajiliwa msimu huu akitokea Simba lakini pia kiungo raia wa DR Congo, Papy Kabamba Tshishimbi, ambaye ameonekana kuimarisha vyema safu ya ulinzi.
 
Lwandamina ameondoka na kikosi chake chote akiwemo mshambuliaji chipulizi Pius Buswita, aliyengara na kuonyesha uwezo mkubwa kwenye pambano dhidi ya Mtibwa Sugar na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora.
Lwandamina amesema wanakwenda Kagera wakitarajia upinzani mkubwa katika mchezo huo lakini wamejipanga kuhakikisha wanapambana nao na kuondoka na pointi zote tatu kama ambavyo wamekusudia.
 
Kagera ni timu nzuri hatuwezi kuidharau hata kama hawajafanya vizuri tangu kuanza msimu huu lakini tunajivunia rekodi yetu ya mwisho tulipocheza hapa ingawa sikuwepo lakini naamini bado kuna wachezaji waliokuwepo na wanataka kufanya vizuri kama ilivyokuwa msimu uliopita,”amesema Lwandamina.
Kocha huyo amesema katika mchezo huo atahakikisha anapanga kikosi chake kamili ili kuhakikisha wanapata ushindi wa mapema utakao wahakikishia pointi tatu za kwanza kwenye mechi zao mbili za Kanda ya Ziwa.
 
Kwaupande wake kocha wa Kagera Sugar Mecky Maxime, amewakaribisha Yanga, na kuwataka watarajie kupokea kipigo wasichokitegemea.
Maxime amesema wamedhamiria kuzinduka baada ya kufanya vibaya kwenye mechi tano za ligi zilizopita na hilo linawezekana kutokana na mikakati waliyojiwekea tangu walipocheza mechi ya mwisho dhidi ya Azam FC.
 
Kocha huyo amesema pamoja na kushindwa kufanya vizuri lakini hatobadilisha kikosi chake sana kama ilivyokuwa msimu uliopita na ataendelea kumtegemea kipa mkongwe Juma Kaseja pamoja na nahodha wake George Kavila ambao wameonyesha uwezo mkubwa wa kupambana na kuipigania timu yao.
Maxime amesema anachokihitaji kesho ni ushindi na watafanya hivyo lengo lao ni kuzinduka kutoka kwenye nafasi mbaya waliyopo hivisasa na kuanza kukimbilia nafasi za juu ambazo ndiyo wamepania kufika huko.
 
Mechi kubwa, lakini uwezekano wa Liverpool kushinda bila ya Sadio Mane ni mdogo sana. Wanakuwa na mashambulizi makubwa wakiwa na Mane dimbani
Mashabiki wa United wanatamani kuona timu yao itakavyoikabili Liverpool. Ungependa kufikiri, kikosi walicho nacho na nguvu ya mashambulizi watakayolazimika kuitumia. Lakini mara kadhaa wamekuwa wakipaki basi, kwa hiyo tunasubiri tuone kitakachotokea. Ni mechi kubwa kwa Romelu Lukaku. Sasa yupo na ni timu kubwa dhidi ya timu kubwa.
Manchester United ni timu bora lakini faida ya Liverpool kuwa nyumbani inaweza kuwapa sare.
 
Ni vigumu kubashiri timu ipi itatoka kifua mbele, Liverpool wakipewa 13/8 na Manchester United 17/10, wakati zikipewa uwezekano wa 12/5 kupata sare.
Romelu Lukaku kufunga goli la kwanza 7/2 na Daniel Sturridge ndiye anayeaminika kuwa mchezaji hatari kwa Liverpool akipewa 5/1 kufunga goli la kwanza.
 
Jose Mourinho amethibitisha nyota wake, Lukaku yupo kamili kuwakabili Majogoo
Jose Mourinho amethibitisha kwamba kapteni wa Manchester United Michael Carrick hatakuwepo siku ya Jumamosi dhidi ya Liverpool kwenye Ligi Kuu ya Uingereza, lakini mfungaji wao bora Romelu Lukaku yupo kamili.
 
Carrick amekosa michezo miwili iliyopita dhidi ya CSKA Moscow and Crystal Palace kwasababu ya majeruhi, yanayomfanya kuendelea kuuguza, Paul Pogba na Marouane Fellaini pia watakosekana kutokana na matatizo ya njama za paja.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa Habari huko Aon Training Complex, Jose ametoa taarifa kwa waandishi kuhusu majeruhi kwenye timu yake, "Michael Carrick? Inajua hawezi kucheza. Najua kwamba, Lukaku yupo fiti na hivyo ndivyo ilivyo.
 
Kocha huyo hajazungumzia kuhusu afya ya Fellaini, ambaye alipata majeruhi kipindi anaitumikia timu yake ya Taifa ya Ubelgiji Jumamosi iliyopita. Chama cha mpira cha Ubelgiji kimeripoti kiungo huyo amepata jeraha la goti.
Marcos Rojo na Zlatan Ibrahimovic wanaendelea kuimarika taratibu kutokana na majeruhi yao ya muda mrefu waliyoumia robo fainali ya Uropa msimu uliopita dhidi ya Anderlecht
 
Arsenal bado hawajashinda mechi ya ugenini kwenye Ligi Kuu Uingereza msimu huu, Wamepoteza mechi mbili na sare
Watford wanakuja kwa kasi Ligi Kuu msimu huu baada ya kupata pointi katika mechi ambazo walikuwa katika nafasi kubwa ya kufungwa. Walikuwa wameshakubali kipigo cha 2-0 dhidi ya West Brom, lakini waliamka kipindi cha pili na kupata sare ya 2-2.
 
Back
Top Bottom