Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa ufupi Watford wameanza vema msimu na timu yao inaonekana kuwa tayari kwa vita ya kukwea juu kwenye msimamo wa ligi.
Lakini pia bado Watford hawajashinda mechi msimu huu. Walipata sare dhidi ya Liverpool na Brighton, lakini pia walichezea kichapo kizito mikononi mwa Manchester City.
 
Arsenal hatimaye waliweza kusimama tena baada ya kuanza vibaya msimu huu. Gunners walipoteza mfululizo mechi dhidi ya Stoke City na Liverpool wiki tatu za mwanzo, lakini mambo yanaonekana kuwa mazuri kwao sasa baada ya kushinda mechi tatu na sare moja katika mechi nne. Bado hawajaruhusu goli tangu kipigo cha kudhalilisha cha 4-0 katika Anfield.
 
Watford waliifunga Arsenal 2-1 katika uwanja wa Emirates mechi ya msimu uliopita kukomesha mendo wa vipigo saba mfululizo Ligi ya Uingereza.
Mechi tisa za mwisho baina ya timu hizo kwenye michuano yote kulikuwa na wastani wa zaidi ya magoli 2.5.
Arsenal wameshinda mechi zote 5 walizocheza Vicarage Road na kufunga magoli yasiyopungua mawili kila mechi.
 
Inatarajiwa kuwa mechi ya kuburudisha kila timu ikiwa inataka ushindi wa kwanza nyumbani na ugenini katika kampeni za msimu huu.
Timu zote zina kiwango kizuri cha kufunga magoli, kwa hiyo tunatarajia kuona magoli mengi, timu zote zitafunga.
Watford inaonekana kuwa timu iliyokamilika na uwezo wa kujibu mashambulizi mara moja wanapofungwa.
Arsenal wanayo nafasi kubwa ya kushinda mchezo huu licha ya kuwa ugenini.
 
Screenshot_2017-10-14-14-08-47.png
 
Back
Top Bottom