Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ni miaka michache tu tangu kuingia kwa simu za mikononi duniani lakini tayari zimeleta utumwa mkubwa wa kimaisha na kifikra kiasi kwamba baadhi ya serikali duniani na kampuni binafsi zimeingilia kwa kuweka sheria kwamba matumizi ya simu hayatakiwi kazini kwani yanasababisha kazi zisiende, huko china tayari wamefungua vituo vingi vya kuwasaidai watu ambao wamepata addiction hizi sa simu na intanet..
 
.. lakini pia mahusiano ya kimapenzi kuharibika sababu ya mtu kukaa kwenye simu muda wote bila kuzungumza na mwenza, kushindwa kuendela binafsi kwa shughuli zako za kiuchumi na kijamii kwa kupoteza muda mwingi sana kwenye simu badala ya kushughulika na maisha, kukosa fursa kwa kushindwa kuwasiliana na watu kwenye usafiri kama mabasi au daladala, uvivu wa kupitiliza kwa kushindwa kufanya kazi za nyumbani kama kupika, kufua, kufanya usafi na kadhalika.
 
kwa tafiti ndogo tu wahanga na watumwa wa simu ni vijana zaidi kuliko watu wenye umri mkubwa, yaani zaidi ya 58% ya vijana wana utumwa huu.
sasa kama umebahatika kuingia kwenye makala hii na kusoma basi hizi ndio dalili kwamba wewe ni mtumwa wa simu na unahitaji matibabu ili uweze kurudi katika hali yako ya kawaida.
 
ukikaa sehemu unasubiri kitu lazima utoe simu; hii inaweza kua kwenye foleni ya benki, darasani unasubiri mwalimu aje, kwenye dalalala au basi unaenda sehemu, kikao kinakaribia kuanza, na kadhalika lakini kabla simu hazijaja watu walikua wanatumia nafasi hizo kufahamiana, kuangalia mazingira ya nje kama utaona fursa, kuongea na wafanyakazi wenzao, kuongea na wanafunzi wenzako kuhusu somo husika na kadhalika lakini kwa sasa hali ni mbaya kiasi kwamba hata kama kikao kinaendelea, mwalimu anafundisha watu bado wanaangalia simu zao.
 
unapoteza muda mwingi kuangalia post kwenye intaneti; umekaa sehemu unatoa simu yako unaingia facebook au instagram na kuanza kuperuzi kwa muda mrefu kwenda chini bila kungalia chochote cha maana na kila baada ya dakika kadhaa unafungua kuangalia kama kuna post mpya na wewe uwahi kutoa maoni yako..lakini pia ukiona hakuna jipya unahamia kwenye mitandao mingine ya kijamii kutafuta jipya na ukikosa kabisa unaweza kuingia you tube na kupotelea huko.
 
unabeba chaja ya simu popote unapoenda; usisingizie kuisha kwa betri hapana wewe ndio unamaliza moto wa simu kwa zaidi ya 50% ya moto wote ndani ya saa moja ya siku inapoanza kwa kufungua vitu vingi sana ambavyo vinakula moto..kwa hali ya kawaida ukiamka na simu asubuhi ukawa bize na shughuli zako na kuitumia kupokea simu na kujibu meseji muhimu itafika jioni bado simu itakua ina moto lakini kama muda wote unayo simu lazima itazima mapema lakini pia jiulize kwanini ukiwa na simu ndogo pembeni isiyo na intaneti huimalizi chaji?.
 
kuisha kwa chaji ya simu yako kunakukosesha raha; simu kuisha chaji sio mwisho wa dunia hasa kama hutegemei simu yeyote muhimu kwa siku hiyo, badala ya kuchanganyikiwa na kuanza kutafuta chaja iko wapi basi achana nayo upate muda wa kufanya mambo mengine na kupumzisha macho yako.
 
unalala na kuamka na simu; mpaka usiku wa manane umeshazima na taa ya chumbani bado macho yako yako kwenye simu na muda mwingine unasinzia bila kujua simu uliiacha wapi lakini ukiamka asubuhi saa moja ya kwanza lazima upitie kila kitu kwenye simu yako kabla ya kuamka na kwenda kuoga na kujiandaa.
 
simu yako inakusumbua wakati wa kuendesha gari; ukiwa unaendesha gari meseji zinazoingia zinakupa muwasho wa kutaka kujua ni nani matokeo yake unajikuta unachati huku unaendesha gari lakini pia ukiwa kwenye foleni lazima uchukue simu uangalie wakati kuna mambo mengi unaweza kufanya kama kusikiliza radio ya gari au kuzungumza na watu ambao uko nao. angalizo; hii ni hatari na imeua watu wengi sana.
 
watu wanaokuzunguka huenda wanakwambia; wazazi wako wanakwazwa sana na kukuona muda mwingi uko kwenye simu, rafiki zako na mchumba wako pia wanakwambia kwamba hupati muda wa kuongea nao sababu ya simu, muda wa kula au kuangalia tv wewe umeshika simu unajibu sms.
 
simu yako inafanya ushindwe kusoma; kama wewe ni mwanafunzi na unajikuta muda wote unasoma huku unaangalia na kujibu meseji za kwenye simu basi ujue umeshageuka mtumwa na utajikuta unasoma vitu vichache sana yaani kama ukipanga kusoma masaa mawili basi nusu saa tu ndio umesoma na saa moja na nusu umeitumia kwenye simu.
 
hisia kwamba simu yako inaita zinakundama; kama kuna muda unasikia simu yako inaita au unapata hisia kwamba simu yako inatoa vibrations halafu ukiangalia hakuna kitu basi ujue imeshakukamata mpaka kwenye mishipa ya fahamu na ndio maana unapata hizo hisia za uongo kwamba simu inaita.
 
unaishi maisha ya kwenye mitandao ya kijamii; unahisi kwamba idadi ya likes unazopata na comment unahisi zinafanya kazi kwenye maisha ya kiuhalisia yaani ukipost ukapata likes nyingi sana unahisi maisha umeyamaliza kabisa kumbe una mambo mengi sana ya muhimu hujayafanya maishani mwako.
 
muda mwingi unaangalia kama kuna ujumbe mpya au notifications; simu yako haijaita lakini kila baada ya dakika tano unatoa kuangalia kama kuna kitu kimekupita kwenye mitandao ya kijamii na usingependwa kuachwa nyuma kabisa lakini pia meseji ambazo hajizajibiwa zinakuwasha kiasi kwamba uko radhi uwahi google kutafuta jibu uweje kukoment mapema.
 
muda mwingi unaangalia kama kuna ujumbe mpya au notifications; simu yako haijaita lakini kila baada ya dakika tano unatoa kuangalia kama kuna kitu kimekupita kwenye mitandao ya kijamii na usingependwa kuachwa nyuma kabisa lakini pia meseji ambazo hajizajibiwa zinakuwasha kiasi kwamba uko radhi uwahi google kutafuta jibu uweje kukoment mapema.
 
Back
Top Bottom