Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mlinzi wa Kagera, Juma Nyosso amekiri kuwa uwezo mkubwa wa Ibrahim Ajib ndiyo sababu ya wao kupoteza mechi dhidi ya Yanga
Nyosso ambaye amewahi kuvitumikia klabu za Simba na Mbeya City kwa miaka tofauti tofauti amesema kuwa walijipanga kumkabili Ibrahim Ajib asisababishe madhara katika lango lao lakini ilishindikana baada ya kuwazidi ujanja
 
Katika mechi hiyo Ajib alifanikiwa kufunga goli moja na kupika lingine lililofungwa na Obrey Chirwa katiak ushindi wa goli 2 kwa 1 dhidi ya Wana sukari hao wa Kagera
“Mechi ilikuwa nzuri na yenye upinzani mkubwa lakini mchezaji wa Yanga ambaye alitupatia shida sana kumkaba alikuwa ni Ajibu.
“Tulijitahidi kumzuia lakini mwisho wa siku akatuumiza lakini hivyo ndivyo soka lilivyo, tumekubaliana na matokeo na sasa tunajipanga kwa ajili ya mechi zetu zijazo,” alisema hivyo Nyosso katika mahojiano na gazeti la michezo, Champion.
 
tumblr_ow8fh6ln5X1wbo47so3_540.jpg




tumblr_ow8fh6ln5X1wbo47so2_540.jpg
 
Back
Top Bottom