Katika mechi hiyo Ajib alifanikiwa kufunga goli moja na kupika lingine lililofungwa na Obrey Chirwa katiak ushindi wa goli 2 kwa 1 dhidi ya Wana sukari hao wa Kagera
“Mechi ilikuwa nzuri na yenye upinzani mkubwa lakini mchezaji wa Yanga ambaye alitupatia shida sana kumkaba alikuwa ni Ajibu.
“Tulijitahidi kumzuia lakini mwisho wa siku akatuumiza lakini hivyo ndivyo soka lilivyo, tumekubaliana na matokeo na sasa tunajipanga kwa ajili ya mechi zetu zijazo,” alisema hivyo Nyosso katika mahojiano na gazeti la michezo, Champion.