Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwanini Mlo Kamili Ni Muhimu Kwa Afya Ya Kinywa?
Kila mara unapokunywa ama kula kitu chochote cha sukari, meno yako hushambuliwa na tindikali (asidi) kwa muda kadiri ya saa moja. Hii ni kwa sababu sukari iliyopo kwenye hicho ulacho ama unywacho hutumiwa na bakteria walio katika utando mlaini ulio kwenye meno (Plaque) kutengeneza asidi.
 
We bana kwa kunitilia kauzibe, kila kona yani! Hapa unachofanya ni kunicheleweshea riziki yangu tu, lakini haitapotea! [emoji23][emoji23][emoji23]
Mimi huyu? Nakuzibia ridhiki? Mimi? Wiki yote hii siyo mimi ninayekujengea mazingira mazuri ya kuvunja zizi mpaka jana ukanilalamikia? Come on maaaaaan!!! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hivyo ni muhimu kuwa na vyakula vya sukari wakati wa milo rasmi kama vile mchana na usiku tu ili kupunguza muda ambao meno yako yatakua yanashambaliwa na tindikali itokanayo na kutumia vitu vya sukari.
 
Screenshot_2017-10-19-19-41-25.png
 
Halikadhalika vyakula vyenye asili ya tindikali vinaathari pia, hii ni kwasababu tindikali huweza kuondoa tabaka la nje la meno(enamel) na kuacha tabaka la katikati (dentine) likiwa wazi. Hii huweza kuyafanya meno yaume pia.
 
Je Vyakula Na Vinywaji Husababisha Meno Kulika?
Ndio. Vyakula na vinywaji vyenye tindikali huweza kusababisha meno kulika kwani tindikali huweza kuondoa gamba la nje la meno (enamel). Ifuatayo hapa chini ni orodha ya pH ya baadhi ya vinywaji na vyakula. Chakula ama kinywaji chochote ambacho pH yake ni pungufu ya 5.5 huweza kusababisha meno kulika..
 
Je Ninaweza Kula Vitu Vyenye Sukari?
Kumbuka suala kubwa hapa si kiwango cha sukari una kula au kunywa, bali ni MARA NGAPI una kula ama kunywa. Vitu vya sukari vinaruhusiwa lakini ni muhimu kuvitumia wakati wa milo rasmi tu. Halikadhalika ikumbukwa kwamba vyakula vya sukari vina madhara mengi mengine mwilini kama vile magonjwa ya moyo na kusababisha kuwa na uzito uliopitiliza.
 
Je Ni Kinywaji Ninapaswa Kunywa?
Maji safi na salama na maziwa ni vitu vizuri kwa kunywa kwani ni rafiki wa meno yako. Ni vizuri pia kunywa juisi za matunda wakati wa milo rasmi na kama unakunywa kati ya mlo mmoja na mwingine, Jaribu kuchanganya na maji ili kupunguza kiasi cha sukari ambacho kinaweza kukutana na meno yako
 
Kula na kunywa vitu vya asidi (tindikali) kwa hakika hudhoofisha tabaka la enameli kwenye meno yako. Kupiga mswaki mara tu baada ya kula vitu hivi vya tindikali huweza kusababisha sehemu ndogo ndogo za tabaka la enameli kuondolewa na mswaki, hivyo inashauriwa kuwa mara ulapo ama unywapo vitu vya asidi kusubiri angalau saa moja ndipo upige mswaki.
 
Kwa hakika ni muhimu kupiga mswaki wakati wa usiku kabla ya kwenda kulala. Hii ni kwa sababu utokaji wa mate hutumika kama namna ya kusafisha kinywa wakati wa usiku hupungua na hivyo kuacha kinywa katika hali hatarishi kwa kutoboka meno.
 
Back
Top Bottom