Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

73096c2d3bd463176f0300d6779d4edb.jpg
 
Boga ni tunda ambalo watu wengi wanalipuuzia.Ni tunda lenye virutubisho vingi na lina faida nyingi kiafya.Tunda hili ni chanzo kizuri cha virutubisho aina ya BETA CAROTENE ambavyo vinafanya boga kuwa na Rangi ya njano.Pia ndani ya tunda hili kuna virutubisho vingine kama potassium,Vitamin c,vitamin E,na madini ya chuma kwa wingi.
 
SHINIKIZO LA DAMU
Boga lina kiwango kikubwa cha Potassium ambayo husaidia kupunguza Kiwango cha Madini ya sodium mwilini ambayo hupelekea kuongezeka kwa shinikizo la damu(high blood pressure) Kwa hiyo boga ni mojawapo ya vyakula muhimu kwa mtu mwenye presha ya kupanda.Vyakula vingine vyenye Potassium nyingi ni kama AVOCADO,NANASI,NDIZI MBIVU,NYANYA,MACHUNGWA NA SPINACH
Pia potassium inasaidia kuukinga mwili dhidi ya magonjwa ya moyo,kiharusi(stroke) na tatizo la mawe kwenye figo
 
Back
Top Bottom