Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Screenshot_2017-10-22-21-19-41.png
 
Netiboli hiyo inaweza isichezwe. Hii barua hapa chini hujaiona? Tunasubiria majibu kutoka chama cha soka UK [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
*************************************

KAMATI TENDAJI,
CHAMA CHA SOKA (UK)

*YAH: NIA YETU YA KUTOONEKANA UWANJANI 5 NOV, 2017*


Rejea kichwa cha habari hapo juu.

Sisi kama mashabiki wa Arsenal, hadi sasa tumekumbwa na *Taharuki* kubwa kufuatia *mambo yasiyoeleweka* ambayo yamekua yakifanywa na hii timu ya *Man City*.

Kuanzia msimu huu uanze hatujui hasa hawa Man City wana Mpango gani.

Ilianza kama masihara hivi, *Liverpool wakala 5*

Wakaja *Feyenoord wakala 4*

Wakaja *Watford wakala 6*

Wakaja *Crystal palace wakala 5*

Juzi hawa wenzetu ambao tulikua tunawategemea *Stock city wakala 7*[emoji26]

Sasa sisi tunaona namba inazidi kuongezeka tuu na hatujui nia hasa ya hawa jamaa ni nini.

Sasa *sisi ni watu wazima na tunafamilia zetu nyumbani na wake zetu wanatuheshimu*,...

tumekaa tukatafakari tumeona bora tuwaandikie barua nyinyi chama cha soka cha uingereza, kwamba tunaomba tuu muwape hao Man City hizo point 3, timu yetu haitakuja uwanjani hiyo tarehe 5 November.


*Kwani Point 3 kitu gani bwana? Shida ni yale Magoli* Wapeni tuu hizo point 3 sisi tumekubali.


Kwa namna hali ilivyo, namba ya Juzi ilikua goli 7! Sasa hatujui wana mpango gani na sisi maana *hadi sasa hawaeleweki*

Au wanataka kutupiga *Course work*, maana wenzetu ndo hao washapigwa *wiki*

Mwisho tunawaomba mufikirie iwekwe sheria ya *KNOCK ~ OUT* kama kwenye ngumi.Yani pale kwenye ngumi ukiona ngumi zimekuzingua, ukinyoosha mikono juu, basi pale pale *Game over!*,na ushindi anapewa mpinzani.

Sasa na huku kwenye mpira muweke hiyo, Timu ikishaona imezidiwa *wakae chini timu nzima pale pale uwanjani*, na game iishie pale pale. Sio kuendelea kushindiliwa magoli.

Tunaoumia ni sisi Mashabiki huku mtaani.

Ni sisi Mashabiki wa Arsenal wa Tanzania
Ahsanteni
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Back
Top Bottom