Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

1.Usitunze hela nyingi benki kwa muda mrefu labda ya biashara au tahadhari.
Hapa mwandishi anajaribu kuelezea kwamba ukiweka hela benki inazidi kushuka thamani na pia itakuwa inapungua kwa sababu benki wanakata tozo la kukutunzia hela yako.Hata kama utaweka kwenye akaunti yenye riba basi riba yenyewe haizidi asilimia nne(4%) baada ya miezi mitatu.
 
3.Jijengee tabia ya kununua hisa.Mwandishi alielezea kwa mapana sana sehemu hii na kusema kwamba kuna makampuni mengi sana yanauza hisa.Cha msingi ni wewe ufanye utafiti ni kampuni ipi inafanya vizuri kwenye soko ili nawe uweze kununua hisa zao.Kwa wake ambao hawaelewi inakuwaje ni hivi;ukinunua hisa kwenye kampuni fulani basi nawe unakuwa mmiliki wa ile kampuni.Kila mwisho wa mwaka kunakuwa na gawio la faida iliyopatikana kutokana asilimia ya hisa zako ulizonunua.Wenye hisa nyingi wanapata gawio kubwa na kinyume chake.Kama kampuni imepata hasara basi kunakuwa hamna gawio labda ukitaka uuze hisa zako kwa mtu mwingine kwa bei ya juu kuliko uliyonunulia.
 
6.Usiwekeze kwenye makampuni madogo,wekeza kwenye kampuni kubwa.Makampuni madogo mara nyingi mwisho wa mwaka hasara zinakuwa nyingi kuliko faida.Anashauri uwekeze kwenye makampuni makubwa kwa mfano hapa kwetu Tanzania kuna kampuni kama ya sigara,mabenki,saruji wanafanya vizuri sana kwenye soko la hisa.
 
Back
Top Bottom