Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Everton wameachana na Ronald Koeman baada ya kipigo cha 5-2 mikononi mwa Arsenal walichokipata Jumapili, ambacho kimeiacha timu hio na ushindi katika mechi mbili tu tangu msimu uanze na ikishuka katika nafasi za timu zenye hati hati ya kushuka daraja.
Koeman alipewa fungu kubwa la usajili wa wachezaji ambapo Everton ilitumia kiasi cha Paundi 142 katika usajili wa wachezaji wapya.
 
Lakini klabu hiyo ya Merseyside imeshindwa kufanya vyema na licha uonyesha dalili za mapema za kufanya vyema. Waliambulia kushinda mara moja tu katika ligi tangu walipopate sare ya 1-1 dhidi ya Manchester City katika mchezo wao wa pili wa msimu.
Walionyesha kiwango kizuri walipopambana na kupata sare dhidi ya Brighton and Hove Albion mnamo Oktoba 15, lakini matokeo mazuri yalishindwa kuendelea na kuipa timu mafanikio.
 
Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain Neymar amedai kuwa kutolewa dimbani kwa kadi mbili za njano dhidi ya Marseille haikuwa haki.
Zikiwa zimebaki dakika tatu alipewa onyo kwa majibu yake baada ya kufanyiwa faulo na Lucas Ocampos, na Mbrazili huyo aliamrishwa kutoka dimbani timu yake ikiwa nyuma kwa mabao 2-1.
Mpira wa adhabu uliopigwa na Edinson Cavani dakika za majeruhi uliwawezesha miamba hao wa Ligue 1 kupata sare, lakini Neymar amekiri kuwa alikasirishwa na hatua zilizochukuliwa dhidi yake katika uwanja wa Velodrome.
 
Neymar, 25, amekiambia Esporte Interativo: "Nadhani mambo yalikuzwa, naam. Haikuwa haki. Mchezo wote nimekuwa nikichezewa rafu. Nina alama tele mwilini mwangu.
"Nilijaribu kuendelea kucheza baada ya kufanyiwa faulo. Lakini nilikerwa zaidi na maamuzi ya refa kwa kunitoa nje."
Licha ya sare hiyo, PSG ipo mbele kwa pointi nne dhidi ya timu inayoshika nafasi ya pili Ligue 1.
 
Mjerumani Sami Khedira alipiga hat trick huku Daniele Rugani, Miralem Pjanic na bao la kujifunga la Samir liliwafanya Juventus kuibuka kidedea kwa ushindi wa mabo 6 kwa 2 dhidi ya Udinesse.
Wakati Juventus wakishinda bao 6 kwa 2, wahenga wa ligi hiyo klabu ya AC Millan walikuwa uwanjani kwao San Siro na kulazimishwa sare ya bila kufungana na sasa wanashika nafasi ya 11 katika msimamo.
 
Tottenham Hotspur 4-1 Liverpool

Tottenham bila huruma waliishughulikia beki mbovu ya Liverpool na kupaa hadi nafasi ya tatu wakiwa pointi sawa na Man United baada ya kushinda 4-1 Wembley.
Nchini Uingereza Tottenham Hotspur wameifikia Manchester United kwa alama ya pointi baada ya Harry Kane(2), Min Son, Delle Ali kuiua Liverpool kwa mabao 4 kwa 2 na kufikisha alama 20.
 
Troyes 0-5 Olympique Lyon

Ligue one nako Lyon walikuwa ugenini dhidi ya Troyes na kuibuka kidedea kwa mabao 5 kwa nunge huku winga wa zamani wa Manchester United akipiga hat trick huku Bertand Troure na Mariano Diaz wakifunga mengine.

Nchini Hispania Kevin Gameiro aliiokoa Athletico Madrid baada ya kufunga bao pekee dhidi ya Celta Vigo, Villareal wakiwa nyumbani waliidondoshea mvua ya mabao Las Palmas baada ya kuichapa bao 4 kwa nunge.
 
Wakala wa Zlatan Ibrahimovic Mino Raiola amedai kuwa straika huyo wa Manchester United bado ana miaka isiyopungua mtano mbele yake kucheza.
Mchezaji huyo wa zamani wa Paris Saint-Germain na Barcelona, ametimiza miaka 36 mapema mwezi huu, na amekuwa nje ya dimba tangu Aprili kwa sababu ya majeraha.
 
Back
Top Bottom