Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

watoto na watu wazima wenye tatizo (bawasiri)wameota kinyama sehemu ya kutolea haja kubwa, wanapata maumivu wakijisaidia, wajipake sehemu ya haja kubwa kabla na baada ya kupata haja kubwa ili ilainishe mishipa!
 
Tiba ya vidonda vya tumbo; Matumizi ni kutia vijiko 2 vya chakula katika uji mara mbili kwa siku kwa muda wa siku 90.
Mafuta ya zaituni hutumika kama huduma ya kwanza kwa aliyekunywa sumu kwa kunywa, na kwa mwenye ganzi au kiharusi hutumia kwa kuchua mwilini asubuhi na jioni.
Mafuta ya zaituni hutumika katika kuua wadudu wabaya walioko tumboni kwa njia ya kunywa kijiko kimoja mara kwa siku kwa muda wa siku saba.
 
Mafuta ya zaituni huongeza nguvu za kiume kwa kunywa kijiko kimoja kwa siku pamoja na kuuchua uume mafuta yaliyochanganywa na vitunguu swaumu kwa muda wa siku saba hadi kumi na moja.
Tiba ya ugonjwa wa kusahau:

paka katika paji la uso kutwa mara mbili pamoja na kunywa kijiko kimoja cha chai mara moja kwa siku kwa muda wa siku 7 hadi siku 11.
Tiba ya degedege:

hutumika kupakaa mwili mzima mafuta marambili kwa siku kwa muda wa siku 7 hadi siku 21.
Kukojoa kitandani:

kupakaa mafuta ya zaituni mwili mzima kutwa mara mbili huku akilamba matone mawili kwa muda wa siku 7 hadi siku 21.
HII NI SAYANSI YA MIMEA
 
e9cec144f39075325607ad5b4b6a7005.jpg


Muwe na Jumanne Njema wapendwa.
 
7. Inapambana na sumu kwenye ngozi
8. Inachelewesha kitendo cha ngozi kuzeeka haraka kwa kuwa inapambana na kuondoa sumu kwenye ngozi. Ina kitu kinaitwa Polyphenols ambacho kazi yake ni kuchelewesha kitendo cha kuzeeka kwa njia ya kuondoa sumu ambazo zinafanya ngozi kuchakaa haraka.
9. Ina Vitamin A, D, E na K zinazosaidia kuzuia ngozi kupatwa na sumu
10. Inasaidia katika uponyaji wa vidonda kwa haraka na kuondoa mabaka au madoa kwenye ngozi
11. Nzuri kwa aina zote za ngozi, hasa zaidi ngozi kavu
 
Kwa wale ambao tuna nywele asilia a.k.a natural hair,tayari tunafahamu changamoto kadhaa tunazokumbana nazo.Kwa wale mnaofikiria kuanza kuwa na nywele asilia,karibuni sana tuendelee kujuzana namna ya kutunza nywele zetu kama tulivyopewa na Mungu.
 
leo,nitakwenda kuzungumzia vitu vya kuzingatia ili kuikuza nywele yako asilia kwa haraka zaidi.Je,unazifahamu nywele zako vizuri?Una nywele za aina gani?Zina tabia gani?Zinataka nini?
 
Kuzikubali kama zilivyo na kuzipenda.

Utasikia ..hiki kipilipili changu ni steelwire ya kimataifa, ..hakitikisiki hata upepo wa dunia yote ungevumia pande hizi.Mwingine oh..nywele zangu kama miti ya mibuyu kichwani…hazishikiki.Tatizo ni kwamba hamjafahamiana vizuri yani wewe na nywele zako.Hata mimi niligombana nazo sana huko nyuma kabla ya kuzielewa vizuri.Jenga mahusiano mazuri tu na nywele zako,zielewe,ukifikia hapo utaanza kuzipatia hata hazitakusumbua.
 
Usafi wa ngozi ya nywele na nywele zenyewe.

Nywele zenye afya huanzia kwenye ngozi safi ya nywele.Nafahamu unataka nywele zako zisidumae kwa hiyo zioshe vizuri.Wakati uliopita nilizungumzia kuziosha kwa product zilizo rafiki( ‘friendly’) .Ngozi safi ya nywele itasababisha nywele kupata njia ya kujitokeza nje kwa urahisi.Unapoziacha chafu,ule uchafu unaziba matundu ya nywele zako na kuzuia njia,kama ambavyo matundu ya uso yakiziba unapata machunusi maana uchafu unajaa basi kwa nywele hazitakua vizuri.
 
Linda unyevu wa nywele zako

Kila mtu akisikia kiu hunywa maji.Nywele zako zinahitaji kulindwa zisisikie kiu.Unapoziosha,yale mafuta asilia ya kuzilinda huondoka na uchafu.Nywele inabaki ikiwa na udhaifu fulani maana haiwezi hata kushikilia hayo maji yaliyopo vizuri,na zikikauka zinakua kavu sana.Ni vizuri kabla hazijakauka vizuri,ukazi-’condition’.Kwa nywele ambazo ni nyepesi na chache,pia kuna product za kuzisaidia ziweze kutunza vizuri unyevu na hivyo kuwa na afya nzuri.
 
Zifahamu nywele zako

Yani hapa ndo shule ilipolalia kabisaa maana ukizijua tu basi utazihudumia kwa usahihi.Unatakiwa kuangalia namna gani nywele zako zinanyonya unyevu.Unajuaje?

Chukua kikombe,kijaze maji safi.Ukipata glass itakuwa vizuri zaidi.

Chomoa unywele mmoja kichwani,hakikisha unatoka na kale kamzizi kake keupe keupe hivi.
 
Tumbukiza unywele wako kwenye glass yako ya maji hakikisha imeingia yote.Kama ikizama hapo hapo na hainyanyuki tena,basi nywele zako zinanyonya unyevu kwa haraka kabisa.Kama inachukua muda kuzama,au haizami kabisa,nywele zako zinanyonya unyevu taratibu au zinanyonya kwa shida.(Wala usihofu,zipo namna ya kuzifanya zinyonye unyevu kwa haraka,tutajuzana.)Ni kwamba ‘cuticle’ zake zimefunga haswa,ndio maana unyevu au maji haviingii kwa haraka.
 
Kwa hiyo ukifanya ‘deep conditioner’ kwa kutumia joto kama la drier lakini uwe moto mdogo sana au ufanye ‘hot oil treatment’ itakusaidia ‘cuticle’kufunguka na unyevu kupita.

Mbadala,unaweza baada ya kuosha suuza na maji ya vuguvugu halafu weka mafuta ya kimiminika.Inasaidia sana.
Mimi nina aina gani?..Nina nywele zinazonyonya unyevu haraka.
 
Back
Top Bottom