Hili ni tatizo la kupenda kula vitu ambavyo si chakula kama vile udongo, mshumaa, mkaa, chaki, karatasi, kucha, majivu na vitu vingine. Mtu yeyote anapotamani kula au kula vitu hivi kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja endapo umri wake ni zaidi ya miezi 24 kwa maana ya miaka miwili ni wazi kuwa ana tatizo la ugonjwa ujulikanao kitabibu kama ‘PICA’.