Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Wasichana wengi wanaokula vitu ambavyo si chakula hukabiliwa na tatizo la upungufu wa madini chuma na zinc mwilini. Hii ni kutokana na lishe duni au kupoteza damu nyingi wakati wa hedhi au upungufu wa madini chuma kutokana ugonjwa wa minyoo ya safura. Ulaji mbaya kama vile kunywa chai yenye majani ya chai au kahawa wakati wa kula huzuia madini ya chuma kufyonzwa au kusharabiwa na kuingia mwilini.