Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa watoto wa kike hii ni hatari kubwa zaidi,kwani simu hizi huenda zikatumika kupanga mipango na wanaume wasio na malengo mema nao na mwishowe wakaingia katika ngono na mimba za utotoni.

Shida nyingine ya simu kwa watoto ni kasumba ya matumizi,simu zinaweza zikawafanya watoto kutokuwa makini na kutozingatia sana masomo yao. Kwani watatumia muda mwingi kuchati na marafiki na kucheza michezo iliyomo katika simu hizi.
 
Intaneti na Mitandao ya Kijamii



Mtandao wa intaneti umekuwa chanzo cha taarifa nyingi duniani kote,mapinduzi ya simu yamechochea upatikanaji wa mtandao huu. Mwanzoni ilikuwa ni lazima uwe na kompyuta,na kompyuta zilikuwa si kwa kila mtu sababu ya gharama kuwa kubwa. Sasa hivi mambo ni tofauti,kompyuta ziko karibu katika familia na watu binafsi. Intaneti nayo ni rahisi kupatikana kwa kupitia simu kwenda kompyuta au modemu.
 
Hii imerahisisha sana mawasiliano na upatikanaji wa habari mbali mbali toka katika mtandao huu. Habari zilizomo katika mtandao wa intaneti hazichujwi kwa kuangalia rika la watumiaji. Humu unaweza ukapata habari nzuri za kuelimisha hali kadharika habari za kupotosha. Kwa namna hii watoto wanaomiliki simu au kompyuta zenye kuunganishwa katika mtandao wa intaneti wanaingia katika hatari.
 
Udhibiti wa Matumizi ya Vyombo Vya Habari kwa Watoto Unahitajika
Serikali iweke mwongozo juu ya udhibiti wa habari zinazowafikia watoto. Zitungwe sheria zitakazodhibiti suala hili ili kusaidia wazazi kulea watoto katika maadili yanayostahili.

Walezi pia wanaweza kuchukua hatua kadhaa za kuongeza udhibiti
 
Kwa watoto wanaoishi na wazazi wao,simu si muhimu sana kwao pia hivyo zinaweza zikazuiwa. Lakini kama zi lazima mtoto awe na simu basi wazazi wazifuatilie kujua nani anapiga na kupigiwa na ujumbe unaotumwa kwa kuzipitia simu moja kwa moja au kutumia programu maalumu katika simu zitakazo tuma ujumbe kwa mzazi au kwa kupata taarifa toka makampuni yanayotoa huduma za simu.u
 
Udhibiti wa Matumizi ya Simu:

Wazazi na Walimu mashuleni wanaweza wakaweka mikakati juu ya udhibiti wa matumizi mabaya ya simu mashuleni kwa kuzuia kabisa umiliki wa simu kwa watoto.

Mawasiliano kati ya wazazi na walimu yapitie kwa simu ya shuleni au walimu pekee.
 
Kwa watoto wanaoishi na wazazi wao,simu si muhimu sana kwao pia hivyo zinaweza zikazuiwa. Lakini kama zi lazima mtoto awe na simu basi wazazi wazifuatilie kujua nani anapiga na kupigiwa na ujumbe unaotumwa kwa kuzipitia simu moja kwa moja au kutumia programu maalumu katika simu zitakazo tuma ujumbe kwa mzazi au kwa kupata taarifa toka makampuni yanayotoa huduma za simu.
 
Udhibiti wa Intaneti na Mitandao ya Kijamii

Wazazi wanaweza wakatumia programu katika simu kufunga baadhi ya taarifa au tovuti zisizohitajika kwa watoto. Watoa huduma wam intaneti wanaweza wakafanya hivyo pia kufunga taarifa ambazo hazihitajiki kartika simu ya mtoto.
 
faith-evans.gif
 
Juhudi za pamoja kati ya Serikali,Wazazi na Walezi Zinahitajika Kudhibiti Hali
Kama taifa kwa ujumla,wazazi na walezi wa watoto wakichukua hatua za pamoja,tutajenga taifa ambalo watoto wanapata kile wanachokihitaji katika malezi katika wakati muafaka. Hii itawarahisishia wazazi na walezi kuwakuza watoto katika maadili sahihi ya jamii zetu.
 
Back
Top Bottom