Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mkuu sijaiona lakini naitafuta mkuu nitakupata mrejesho
JUNIOR MAFIA
Filamu ya Maisha ya Biggie inaitwa NOTORIOUS.

JUNIOR MAFIA ni Kundi ambalo lilikuwa chini ya BIGGIE.

Na kundi hilo lilikuwa na Mlimbwende mmoja pekee ambae ni LIL KIM.

Kwahiyo katika Filamu hii ya kuitwa NOTORIOUS walioigiza hawakuwa Wahusika halisi, yaani kuanzia BIGGIE mwenyewe, FAITH EVANS, PUFF DADDY, kundi la JUNIOR MAFIA, na wengineo wote.

Hicho ndicho nilichokuwa namaanisha.

Bila shaka utakuwa umenipata vizuri sana Kiongozi wangu
 
Pamoja mkuu
T+I+Takers+New+York+Screening+64cTxfuflC2l.jpg
 
Nini tena mkuu
Kiongozi.

Nilipokuwa bado naendelea na NUKUU zako, kati kati ya Uhondo ikabidi nikatishe kisha niendelee na dharura ya ghafla iliyonipata.

Kwahiyo ikabidi niishie kati, kisha nikarudi tena na kuendelea nilipokuwa nimeishia baada ya kumaliza dharura ya ghafla iliyotokea.

Mfano hai ni huu hapa, hizi NUKUU zako Jana nilikuwa sijafika kote huku niliishia kati kati ya Safari.

Kwahiyo leo nimeanzia Safari yangu pale nilipoishia na kuendelea mbele na Safari.

Kama nikifika mwisho wa Safari yangu itakuwa vyema, ila kama itakuwa sijafika mwisho wa Safari yangu, basi hakuna tatizo nitaendelea tena Kesho kunako Majaliwa mpaka nihakikishe nimepitia kila NUKUU bila ya kuipita hata moja.

Mambo mengine yanakwendaje Kiongozi wangu?
 
Kitimoto....

Uipate ile rosti iliyorostiwa mpaka ikageuka kuwa brown, afu pembeni unawekewa pilipili za kukata zile... zimechanganywa zile za kijani na moja inayoelekea kwenye wekundu hiviii. Pemben tena kuna vipande viwili vya ndimu zile kubwakubwa pamoja na chumvi.

Hiyo uipate na dona au ndizi kama 3 hivi zilizokaangwa. Kabla hata hujamaliza kuikagua sahan kama kila ulichoagiza kimefika unaambiwa na mhudumu "naomba unawe".... unamuangalia kidogo usoni then unakinga mikono unanawa, maji vuguvugu saaafi kabisa.

Anamalizaa anaondoka unamsindikiza kidogo na jicho la kiwizi then unairudia sahan yako. Unapiga one touch moja unakamata kipande cha kitimoto kilicholowa rosti zito unakitupia mdomoni na kabla hujatafuna sana unang'ata na kipande cha pili pili. Then baada ya hapo unachukua kipande cha ndimu na kuanza kukamulia taratiiibu kwenye rosti yako huku ukiiangalia kwa madaha beer yako iliyopo pembeni na imefungwa tishu kwa juu.....


*......Itaendelea*
 
Mzazi anakosa kujiamini katika jukumu lake la kumfundisha mtoto kwani anatambua sasa kuwa mtoto ni mjuaji wakati ungine kumzidi,na anaweza kuamua kutofanya hilo jukumu kwa kujua mtoto anafahamu tayari. Wakati mwingine inakuwa si sahihi.
 
Mtoto anatambua baada ya muda kuwa mzazi wake hafahamu mambo mengi na kuwa yeye anafahamu zaidi. Hivyo naye anaacha kuuliza au kutaka kufahamu toka kwa wazazi. Hivyo anaweza akafanya vitu kwa ufahamu wake tu binafsi au kwa kutafuta msaada sehemu nyingine nje na wazazi wake. Na huenda msaada atakao pata ukawa sio sahihi.
 
Ni kitu cha kushangaza kuwa miaka 20 tu iliyopita hakukuwa na TV katika nchi hii ukiachia ile ya Zanzibari (TVZ). Lakini sasa hivi kuna utitiri wa TV kila mahali nchini. Nyingine ni za ndani na nyingine ni toka nje.
 
Vipindi vya TV vinatofautiana na vinatoa habari mbalimbali. Nyingine ni nzuri kwa watoto na nyingine si nzuri sana. Mfano kuna baadhi ya TV za nje ambazo zinaonyesha vipindi vya ngono usiku kwa kutegemea watoto wamelala. Lakini watoto wakijua kuna vipindi hivi huenda wakaamka usiku wazazi wakiwa wamelala na wakaziona. Lakini usiku kwa nchi moja inaweza ikawa mchana kwa nchi nyingine,hivyo hiyo ni changamoto katika kulea watoto wetu.
 
Sia ajabu pia ukakuta TV chumbani kwa watoto siku hizi,hii inaongeza hatari iliyopo katika kuchuja taarifa toka katika TV.

Sinema na tamthilia zimekuwa mojawapo ya vipindi katika TV ambazo wengi wakiwemo watoto wanapenda kuziangalia. Japo vipindi na sinema hizi zinaweka kiwango cha chini cha umri wa waangaliaji,lakini ni ngumu kwa wazazi kusimamia hilo. Hivyo watoto wengi wanapata habari na mafunzo yasiyofaa kwa jamii zetu. Aidha yanakiuka mila,desturi na utamaduni wajamii wanazoishi au zinafundisha mambo ya kikatili kama vile vipindi vya mieleka na sinema na mauaji ambazo zinawajenga watoto katika misingi isiyofaa, kwani kwa watoto hiyo ni halisia na sio maigizo.
 
Simu za Mikononi



Matumizi ya simu za mikononi yameleta mapinduzi makubwa katika jamii zetu kwa kuboresha mawasiliano. Kusambaa kwake kila sehemu nchini hata vijijini kumewezesha mawasiliano ya kibiashara na kijamii kuwa rahisi na kupunguza gharama kwa wengi.

Lakini pia kumeleta mpasuko mkubwa wa kimaadili si kwa watoto peke yake bali hata kwa wazazi wenyewe.
 
Wizi , udanganyifu kati ya wapenzi ni mojawapo tu ya mifano ya matumizi mabaya ya simu.

Siku hizi inakuwa kitu kinachozoeleka kwa watoto kuwa na simu,hata wakiwa shuleni. Kwa maelezo kuwa wazazi wangependa kuwasiliana na watoto wao wakiwa mbali. Ni kweli,hiki ni kitu kizuri lakini kinacholeta shida ni matumizi mabaya ya simu hizi. Mtoto akiwa na simu ataanza kuwasiliana na watu tofauti na si wote kati ya hao ni watu wema.
 
Back
Top Bottom