Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Waweza kujikinga kupata fangasi au kuarakisha kupona fangasi katikati ya vidole vya miguu kwa kutumia pamba? Kwa kunyofoa pamba kidogo na kuiweka katika nafasi baina ya vidole vya miguu kabla ya kuvaa soksi, husaidia kurahisisha hewa kupenya kwa urahisi unapokuwa umevaa viatu.Pia pamba hufyonza unyevu katika sehemu hizi za vidole vya miguu. Hii husaidia kujikinga na fangasi baina ya nafasi za vidole vya miguu, pia huarakisha kupona haraka.
 
Dawa za kupaka zenye steroidi ni zile zenye kutibu magonjwa ya ngozi kukakamaa na kuwa kavu (kwa kitaalam eczema), pia aina nyinginezo za magonjwa ya ngozi yasiyo ya uambukizi. Kama zilivyo dawa nyingine ambazo tunatumia kwa kumeza, dawa hizi za kupaka zenye steroidi huwa na maudhi ya dawa, pia madhara yasiyovumilika zinapotumika vibaya.
 
Kumekuwa na wimbi la matumizi ya dawa za kupaka zenye steroidi miongoni mwa wanajamii bila ya kupata ushauri wa wataalamu wa ngozi.Wengi wa watumiaji huzitumia kama vipodozi. Wahanga wakubwa ni wanawake ingawa na wanaume pia wamekuwa wakijihusisha na matumizi mabaya ya dawa hizi.
 
Madhara wapatayo watu hawa wanaotumia dawa hizi zenye steroidi za kupaka kiholela, ni wazi kwa muonekano wa ngozi zao. Pia kuna madhara mengineyo mengi ndani ya mwili ambayo mtumiaji holela anaweza kupata, hii ni kwa sababu dawa hizi pia zina uwezo wa kusharabiwa mwilini.
 
Dawa hizi za kupaka zenye steroidi huwa hazina madhara endapo mtumiaji atatumia kama alivyoandikiwa na daktari wa ngozi, chini ya uangalizi na ufuatiliaji wa watataalamu wa afya. Dawa hizi za kupaka kwa mfano ni kama Dermovate®, Diprosone®,Sonaderm®,Gentrisone®,Safi®,Elyvate®,Betason®, Betacort® na nyinginezo nyingi.
 
Madhara wapatayo watu hawa wanaotumia dawa hizi zenye steroidi za kupaka kiholela, ni wazi kwa muonekano wa ngozi zao. Pia kuna madhara mengineyo mengi ndani ya mwili ambayo mtumiaji holela anaweza kupata, hii ni kwa sababu dawa hizi pia zina uwezo wa kusharabiwa mwilini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…