Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

678ce61ac5ea3183e39211e8592e863c.jpg
 
b)Matatizo ya kisailolojia
Ubongo huwa na kazi maalum ya kuongoza jinsi viungo vya mwili vinavyofanya kazi, hii ni pamoja na kusimama kwa uume baada ya mhemko kabla ya tendo la ndoa. Kuna baadhi ya mambo yaweza kusababisha mwanaume asihemke na kuendelea kusababisha tatizo kuwa kubwa zaidi. Sababu hizo ni kama ifuatavyo:-
 
Mchanganyiko wa hitilafu katika Ogani na Saikolojia kwa pamoja.

Tunavyoozeeka tatizo hili laweza kuongezeka, ingawa siyo hali ya kawaida mtu anapozeeka. Wazee ni kundi ambalo hutumia dawa za matatizo mbalimbali kwa wingi. Kwa hiyo tatizo hili la upungufu wa nguvu za kiume linapotokea mara nyingi huashiria hali ya kiafya isiyo ya kawaida au kusabishwa na aina fulani za dawa atumiazo mgonjwa. Mara nyingi hutokea kwa wale walio na miaka 60 na kuendelea. Hata hivyo vijana huweza pia kupata tatizo hili.
 
Pia wanaoweza kupata tatizo hili ni kama:-
Wenye matatizo ya kiafya, kama ugonjwa wa kisukari na ugonjwa wa moyo.
Wenye kuendesha baiskeli kwa muda mrefu, uendeshaji wa baiskeli bila kutumia vifaa maalum waweza kusababisha kukandamizwa kwa mishipa ya fahamu na kuathiri mzunguko wa damu katika uume.
 
Matatizo yenye kujitokeza ugonjwa usipotibiwa
Kutoridhika katika uhusiano.
Msongo wa mawazo na wasiwasi.
Sononi.
Kujisikia vibaya mbele ya jamii na kutokujiamini.
Matatizo ya uhusiano au kuvunjika kwa uhusiano.
Kutokuwa na uwezo wa kumpa ujauzito mwanamke.
 
Endapo tatizo hili litajitokeza, usikimbilie kuanza kutumia dawa, au kununua dawa katika famasi bila ushauri wa daktari. Dawa hazitakuwa na msaada endapo chanzo cha tatizo hakijagundulika. Pia matumizi ya dawa yanaweza kukuletea athari nyingine kiafya, kama uchunguzi haukufanyika kwanza.
 
Jiandae kumwona daktari wako, kwa kukusanya taarifa mbalimbali kama dalili za ugonjwa ulizo nazo, listi ya dawa unazotumia, uwe na taarifa muhimu za kukuhusu, ni vyema ukienda na mwenzi wako kwa kuwa atakuwa msaada kwa yale uliyosahau na andaa maswali utakayomuuliza daktari wako.
 
Vipimo mbalimbali vyaweza kutumika ili kugundua sababu ya ugonjwa. Vipimo hivi hujumuisha vile vya kuchunguza mzunguko wa damu katika uume, pia kipimo maalum cha kuvaa nyakati za usiku kuchunguza mara ambazo uume unasimama ukiwa umelala, na vile vya kuchunguza viwango vya homoni mwilini.
 
Pia historia ya mgonjwa itamwezesha daktari kuweza kugundua tatizo la mgonjwa akishirikisha na vipimo mbalimbali tulivyovitaja hapo awali

Daktari ana wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa unapata tiba sahihi kulingana na kisababishi cha ugonjwa na kinachofanya hali kuwa mbaya kama tulivyoona awali.

Kulingana na sababu inayosabisha ugonjwa wa upungufu wa nguvu za kiume, unaweza kutibiwa kwa njia mbalimbali. Daktari wako na mfamasia watakuelezea faida na hasara ya kutumia tiba husika na watajali zaidi uamuzi wako. Pia mawazo ya mwenzi wako yatasaidia ili uweze kupata tiba iliyo sahihi.
 
Back
Top Bottom