Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Dawa za kumeza zinatumika sana katika kutibu upungufu wa nguvu za kiume na zimeonyesha mafanikio makubwa. Dawa hizi ni kama zifuatazo:-

a) Dawa zinazoongeza mzunguko wa damu katika uume,

Tadalafil(Sialis)
Sildenafil (Viagra)
Verdenafil ( Levitra)
Avanafil (Stendra)
 
Tahadhari
Chukua tahadhari kabla ya kutumia dawa yeyote kutibu nguvu za kiume, hata kama ni dawa za kienyeji au zile zinazonunuliwa bila ya kuandikwa na daktari. Wasiliana na mfamasia kwa ushauri zaidi.

Dawa zitumiwapo ovyo zinaweza zisikusaidie kutatua tatizo na zaweza kuwa hatari kama:-
 
Unatumia dawa zenye nitrate-ambazo huandikiwa wagonjwa wenye maumivu ya kifua (angina), kwa mfano Nitroglycerin,Isosorbide mononitrate na isosorbide dinitrate.
Unameza dawa za kusaidia mtiririko wa damu (anticoagulant) au dawa za shinikizo la juu la damu.
Una tatizo la moyo au moyo kushindwa kufanya kazi.
Una ugonjwa wa kiharusi au uliwahi kupata kiharusi.
 
Dawa za homoni.
Dawa kama testosterone yaweza kutumika kwa wanaume wenye upungufu wa homoni hiyo. Kwa wale wenye upungufu wa homoni dawa hii inaweza kuwa tiba ya kwanza

Upasuaji waweza kufanyika endapo mishipa ya damu ya uume itakuwa imeziba na kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.
 
Ushauri nasaha ni muhimu kwa wagonjwa wenye matatizo ya kisaikolojia, ambayo hupelekea msongo wa mawazo, wasiwasi na hata sononi. Daktari wako anaweza kukushauri wewe na mwenzi wako kuonana na mwanasaikolojia au mshauri nasaha kama tatizo hilo linaleta mvurugano katika uhusiano wenu.
 
Back
Top Bottom