Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

MADHARA YA BPH

BPH kama ilivyo saratani ya tezi dume, inaweza kumletea mgonjwa madhara (complications) kadhaa. Madhara hayo ni pamoja na

Mkojo kushindwa kutoka (retention of urine)Mgandamizo kwenye kibofu cha mkojoVijiwe kwenye kibofu cha mkojoUambukizi katika njia ya mkojo (UTI)Madhara katika figo au kibofuShinikizo la damuKushindwa kutoa shahawa kwenye uume (retrograde ejaculation)Nimonia (Pneumonia)Damu kuganda

Baada ya mgonjwa kujihisi dalili zilizotajwa hapo juu, daktari atamfanyia uchunguzi wa mwili kabla ya kumfanyia vipimo zaidi. Vipimo vyaweza kutofautiana kati ya mgonjwa namgonjwa, lakini baadhi ya vipimo ni pamoja na.
 
Marahaba shemeji kipenzi. Kumekuchaje? Nyuki wachavusha maua bado wapo hapo kwako? Jirani yako leo naona kawaamulia kweli kweli !!!
Ukipata pumzi tu ni jambo la kumshukuru Mungu mengine ni madogo.
Nimefikia uwamuzi wa kuhama mtaa na nyumba nauza[emoji23] [emoji23]
Huku kwema sijui huko uliko,jakitoo mzima?
 
1.KUCHUNGUZA TEZI DUME KUPITIA NJIA YA HAJA KUBWA AU DIGITAL RECTAL EXAMINATION (DRE):


Hiki ni kipimo cha kwanza kabisa ambacho mgonjwa hufanyiwa na daktari wake. Ni kipimo kinachoweza kumpa daktari picha ya tatizo na kufahamu kuhusu ukubwa na hali ya tezi dume. Daktari akiwa amevaa glovu huingiza kidole chake cha shahada katika njia ya haja kubwa au puru (rectum) ya mgonjwa kasha kuzungusha zungusha ili kufahamu kama tezi limevimba ama la na pia hali yake kama ni gumu kuliko kawaida ama lina utando na nyama laini.

Nb:kutokana na jinsi procedure hii inavyofanyika siku hizi haifanyiki kwahiyo wanaume kuanzia 50yrs and above mkapime tezi dume
 
2.KIPIMO CHA DAMU CHA PROSTATE-SPECIFIC ANTIGEN (PSA):

PSA husaidia kutofautisha kati ya saratani ya tezi dume na BPH. PSA ni aina ya protein inayozalishwa na seli za tezi dume na kiwango chake huongezeka iwapo kuna saratani ya tezi dume.
 
3.UTRASOUND YA PURU (RECTAL ULTRASOUND):

Kipimo hiki hufanyika iwapo daktari atahisi kuwepo kwa saratani ya tezi dume badala ya BPH. Utrasound ya puru pamoja na kuonesha taswira ya tezi dume ilivyo, pia humuwezesha daktari kuchukua kinyama (biopsy) kwenye tezi dume kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kutofautisha kati ya saratani na BPH
 
5. KIPIMO CHA KUCHUNGUZA KIBOFU CHA MKOJO (CYSTOSCOPY): Kipimo hiki husaidia kuweza kufahamu ukubwa wa tezi, sehemu tezi lilipobana njia ya mkojo na kiwango cha kubana huko. Aidha huwezesha pia kutambua hali ya kibofu cha mkojo ikoje.
 
MATIBABU YA TEZI DUME

Matibabu ya BPH yameganyika katika sehemu mbili, yale yanayofanywa kwa kutumia dawa na yale yanayofanywa kwa kutumia upasuaji mdogo. Aidha matibabu hufanywa kwa watu wenye BPH kubwa zaidi na dalili zinazowaletea usumbufu na kuathiri maisha yao, wakati wale wenye dalili ndogo ndogo hawalazimiki sana kuhitaji matibabu.
 
Back
Top Bottom