Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Screenshot_2017-11-03-18-42-35.png
 
sio siku kadhaa. Kwa hiyo usitegemee kukaa na smartphone yoyote ile ukiitumia sana na ukategemea itakaa na wewe kwa siku mbili bila kuonyesha taarifa(pop-up notifications) kwamba inahitaji chaji au kukwambia inakwenda kuzima. Samsung yupo tofauti kidogo, simu zake za hali ya chini(low end smartphones) mpaka za hali ya juu(high end smartphones) zina battery inayoweza kutolewa. Ni suala la kubadili tu battery na kuendelea na kazi zako kama una battery ya ziada.
 
Ukiwa na smartphone iliyo na battery inayoweza kutolewa, kiukweli faida ni kubwa. Pale battery unayotumia inapochoka, ni suala la kununua nyingine na kubadili mara moja na smartphone yako inarudi katika hali yake ya kawaida. Tofauti na simu isiyoweza kutolewa battery yake, itakubidi kulipia pesa nyingi katika kupata battery nyingine na huwezi badili mwenyewe mpaka upate mtu mwenye utalaamu wa kubadili battery hiyo. Na sio tu kwamba kulipia pesa nyingi katika kubadili battery husika,
 
nyingi ya battery hizi huwa hazitengenezwi na kampuni iliyotengeneza smartphone husika na ubora wake huwa haufanani na ule wa battery halisi ya mtengeneza smartphone hiyo. Kuna mambo ambayo si muhimu san kuzingatia katika chaguo la smartphone ambayo mtu anataka nunua mfano rangi yake, umaridadi wa display na mengineyo, haya si mambo ambayo kila mtu hujali. Inapofika suala la battery bora yenye uwezo kila mtu hujali sana.
 
Sijataja mibadala mingine ambayo inakuepusha na kero ya simu kuzima kila mara kwa sababu ya kuisha chaji.......Power Bank, Huwa sioni kama mbadala bora kwa sababu huongeza mzigo mwingine usio wa ulazima. Inakubidi kubeba simu na power bank kwa wakati mmoja, huondosha uhuru katika matumizi ya simu yako. Battery ya ziada haileti usumbufu wowote zaidi ya kubadili na kuendelea na kazi. Kuna baadhi ya kava za simu ambazo na battery ndani yake inapatia simu yako nishati, hizi kava huwa nene na huongeza uzito katika smartphone, na kuna watu wengine wasiopendelea kabisa kuweka kava katika smartphone, bila shaka hawatotumia kava hii.
 
Teknolojia inabadili asili yetu.
Teknolojia inazidi kukua siku hadi siku, na kwa kasi ya ajabu sana. Kama wanadamu, tunatakiwa tambua ya kwamba " unapotumia sana mawasiliano ya internet na ndivyo unajitenga na mawasiliano ya kidunia(physical interactions)". Teknolojia inatuondoa katika mazingira yanayotuzunguka na kutupeleka katika mazingira ambayo si halisi, tuna marafiki wengi wa mitandaoni kuliko marafiki tulionao shule au kazini. Tunatumia muda mwingi katika smartphones zetu kuliko kuongea na wale wanaotuzunguka.
 
Miaka ya zamani, kabla ya teknolojia kuitawala dunia watu walikuwa wakienda sehemu wasizozijua kwa kuelekezwa na mtu mwingine au kutumia ramani iliyopo katika karatasi. Tofauti na siku hizi, hatujui hata kusoma ramani, tunapata shida kujua alama za barabarani na hatuna muda wa kusoma maelezo yaliyopo njiani na katika majengo. Unaenda sehemu usiyofahamu? Sawa! Google Maps itakuelekeza kuanzia ulipo na upite wapi mpaka kufika unapohitaji kwenda, rahisi sana eeh!
 
Smartphones na wearable devices kama smartwatches na fitness trackers zina uwezo wa kutuambia tumetembea hatua ngapi kwa siku, tumepunguza uzito kiasi gani na mambo mengine mengi mno. Jokofu(fridge) linaweza tuma taarifa katika smartphone yako kukujulisha ni mahitaji yapi yanakaribia kuisha ndani yake, huna haja tena ya kulifungua na kukagua na kupoteza muda. Haya yote ni faida kubwa sana kwetu kwa sababu huokoa muda na kufanya maisha kuwa rahisi mno.
 
Ingawa tuna apps lukuki katika smartphone zetu zinazotuelekeza jinsi ya kula mlo wenye kuleta afya, njia bora za kufanya mazoezi na kujipa mapumziko, jinsi ya kupika chakula bora, namna ya kupangilia muda kwa ufanisi zaidi, jinsi ya kuendesha gari kwa umakini na kufata alama za barabarani na mengine mengi. Lakini afya zetu si nzuri ukilinganisha na watu wa zamani, hatujui namna ya kupangilia muda wetu, ni madereva wabaya na wenye vurugu mno, maisha yetu yana msongo wa mawazo kila kukicha, tofauti kabisa na watu wa miaka ya zamani.
 
Teknolojia imefanya mengi mno katika kumletea mwanadamu maendeleo, ukiangalia maisha ya watu wengi yanaokolewa mahospitalini kutokana ma matumizi ya vifaa vilivyo na teknolojia ya hali ya juu, si shida tena kufanya mawasiliano kokote duniani, uzalishaji umezidi kuongezeka na faida nyingine nyingi nyingi. Lakini, teknolojia hii inatufanya kupoteza maarifa ya kujua kufanya vitu vingi vya msingi(basic things). Kwa nini ufue kwa mkono? Mashine iko pale! huhitaji kujua muelekeo wa unapokwenda, GPS navigator ipo katika gari yako kwa ajili ya kazi hiyo. Changamoto ni kubwa sana katika teknolojia!
 
Back
Top Bottom