Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Yes. Give me your hand....
222a3ecdbbdf32f795fd540ebd783fed.jpg
0847241577275a3117b2057270335068.jpg
 
Kikosi cha Simba kinatarajia upinzani mkubwa kwenye pambano la Jumapili wakati watakapoikabili Mbeya City uwanja wa Sokoine Mbeya
Kocha msaidizi wa Mbeya City, Mohamed Kijuso ameitahadharisha klabu ya Simba, kuwa kujiandaa na kipigo katika pambano lao la Jumapili litakalofanyika kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.
 
Jumla la michezo 7 ya Ligi Kuu Tanzania Bara kufanyika wikendi hii
Michezo hiyo ya Jumamosi itakuwa ni kati ya Singida United itakayocheza na Yanga kwenye Uwanja wa Namfua mkoani Singida wakati Tanzania Prisons itakuwa wageni wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Kagera.
 
Njombe Mji kwa upande wake watakuwa wenyeji wa Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Sabasaba mkoani Njombe huku Mtibwa Sugar ikisafiri kutoka Morogoro kwenda Mtwara kucheza na Ndanda FC kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona. Hizo ni mechi zitakazochezwa saa 10.00 jioni.
 
Jumapili kutakuwa na michezo miwili ya Ligi Kuu ambako Lipuli ya Iringa itakuwa mwenyeji wa Mwadui FC ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Samora wakati Simba itakuwa mgeni wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Mechi hizo zitaanza saa 10.00 jioni.
 
Kocha msaidizi wa Mbeya City, Mohamed Kijuso ameitahadharisha klabu ya Simba, kuwa kujiandaa na kipigo katika pambano lao la Jumapili litakalofanyika kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.
Kijuso ameiambia Goal, wameiona Simba, walipocheza dhidi ya Yanga Jumamosi iliyopita na kubaini mapungufu mengi kwenye kikosi hicho ambacho ameahidi kuyafanyia kazi ili kupata ushindi.
 
Msimu uliopita tulipata sare ya mabao 2-2, kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam, safari hii tunataka kuwafunga mbele ya mashabiki wetu kwasababu dhamira tuliyokuwa nayo ni kupanda kwenye nafasi za juu kama ilivyo kwa timu nyingine," amesema Kijuso.
 
Kocha huyo msaidizi amesema maandalizi yao kwa ajili ya pambano hilo la Jumapili yanakwenda vizuri na kwenye kikosi chao hakuna mchezaji yeyote aliyokuwa majeruhi jambo ambalo linawapa matumaini ya kutimiza ahadi yao kwa mashabiki.
 
Amesema anatambua kuwa Simba ni timu kubwa na inaundwa na wachezaji wenye majina makubwa lakini hilo haliwatishi watakacho kifanya hakitokuwa na tofauti ya kile walichofanyiwa na Yanga na kujikuta wanacheza kwa kuzuia kwa kuhofia kufungwa.
 
Mbeya City, ni moja ya timu ambayo imekuwa na rekodi ya kuisumbua Simba, na mara kadhaa Simba wamekuwa wakipoteza mchezo dhidi ya vijana hao wa Gren City ambao kwasasa wanafundishwa na kocha Ramadhani raia wa Burundi baada ya uongozi kumtimua kazi Kinnah Phiri raia wa Malawi.
 
Back
Top Bottom