Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Screenshot_2017-11-03-18-14-40.png
 
Siku ni hizi kwa wengi ni vigumu kutomiliki power bank yaani betri ya ziada ya kuchajia simu au tableti yako. Umuhimu wa power bank umekua zaidi kutokana na umeme unaoweza kukatika muda wowote ila pia kwa kuwa simu janja zitu zinaweza kuisha chaji muda wowote huku tukiwa mbali na sehemu za kuchaji.
 
Watu wengi wanatumia smartphones kwa shughuli mbalimbali, iwe ni kuperuzi mtandaoni, kusikiliza muziki, kupiga picha, kutuma barua pepe au kuchati. Yote haya hutumia nishati kubwa sana ya umeme katika smartphones. Simu hizi hazina uwezo mkubwa wa kuhimili kukaa muda mrefu ikiwa na nishati huku ukiitumia mfululizo. Hii inapelekea uhitaji wa kuipa nishati(recharge) smartphone yako mara kwa mara. Ukiwa ofisini, nyumbani au popote pale palipo na umeme suala la kuchaji simu ni rahisi tu. Lakini inakuwaje upo porini, au sehemu yoyote iliyo haina umeme kabisa na hauna nishati yoyote mbadala?
 
Si tu uwe katika sehemu isiyo na nishati ya umeme ndipo ushindwe recharge simu yako, kuna wakati umeme hukatika, na suala hili ni kawaida. Ina maana kwamba utakwama katika shughuli uliyokuwa ukifanya. Ni afadhali ukiwa unasikiliza muziki, utaburudika tena baadaye lakini isiwe ni wakati ambao ulikuwa ukisubiri simu muhimu sana na hauna mbadala wa kupata tena mawasiliano. Lakini, pengine ungekuwa simu yenye uwezo wa kubadili battery(removable battery) ungeweza kuepuka zahama hii.
 
Wengi ya watengenezaji wa smartphones walio na majina makubwa kama HTC, LG, Sony, Apple, Huawei, Microsoft na Xiaomi wanaelekeza nguvu zao nyingi katika kutengeneza simu zilizo na battery isiyoweza kutolewa(non-removable battery) kuliko zile zenye battery ya kutolewa(removable battery). Hutamba ya kwamba simu zao zilizo za hali ya juu(high end smartphones) zina uwezo mkubwa kwa kukaa na charge kwa mrefu, muda wenyewe ni masaa,
 
Back
Top Bottom