Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Makampuni makubwa ya teknolojia huuza taarifa za watumiaji wa bidhaa na huduma zao bila kutoa taarifa yoyote kwa watumiaji. Na katika wakati huohuo, ukisoma sera za ukusanyaji, uhifadhi na matumizi ya taarifa za mtumiaji(Privacy Policy) zinaeleza wazi kabisa kwamba taarifa zote zinazomuhusu mtumiaji wa huduma zao ni siri na zitatolewa pale tu mtumiaji huyo atapoidhinisha. Matoleo(versions) ya sasa ya Android OS na iOS yana mfumo ambao unalinda taarifa zako zote katika smartphone yako kutoweza kuonekana na kutumika na mtu yoyote isipokuwa wewe tu, mfumo huu unafamika kama encryption.