Njia Rahisi Ya Kuwezesha PC Yako Kuwa Wi-Fi Hotspot
Hotspot ni huduma inayopatikana mahali fulani (physical location) inayomuwezesha mtumiaji mwenye kifaa cha kielectroniki kilicho na uwezo wa kutumia wireless connection, kuweza kujiunga na kutumia internet. Kwa kifupi, ni mahali ambapo unaweza unga laptop, tablet computer au smartphone yako na kutumia internet bila ya kuunga nyaya zozote (wirelessly). Mara nyingi hotspot hupatikana maeneo kama ya vyuo, mahotelini, sehemu za wazi za kujipumzisha au migahawani. Kutokana na ukuaji wa teknolojia, siku hizi smartphone zina uwezo wa kuwa Wi-Fi Hotspot pia.