Unapokuwa huezi kulala vizuri usiku , fikiria kilichofanyika jioni yake na kujaribu kufahamu kitu gani kilikwenda vibaya. Unaweza kuanza kufikiria huenda nilienda kulala mapema. Au nibadilishe mto, au ilikuwa baridi, au ilikuwa joto sana
Katika makala hii utajifunza kitu gani hasa cha kufanya asubuhi, mchana na jioni ili kukuwezesha kulala usingizi mzuri na kuamka na nguvu ya kutosha kila siku.
Tuanze mwanzo kabisa– mission yako ni kutaka kulala vizuri na kuamka vizuri bila ya kuconfuse mwili wako. Ni vizuri kama utaamka muda huohuo kila siku ili kupanga kulala kwako na kuamka kwako.