Unachopaswa kufahamu ni kwamba bidhaa za dawa na vipodozi ni miongoni mwa bidhaa ambazo zinasimamiwa na sheria kali za nchi sehemu mbalimbali duniani. Kwa Tanzania zinasimamiwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) ambayo ndiyo inakagua, kusajili, kupitisha mabadiliko na kusimamia matumizi yake. Mabadiliko yoyote katika bidhaa hizo ni lazima yajulikane na TFDA na yapitishwe, pia kampuni halisi inayotengeneza dawa na vipodozi hivyo itawatangazia wateja wake ili kuwajulisha juu ya mabadiliko hayo na kuwatoa hofu.