Madoadoa na makovu hutokea wakati wa kupona kwa vidonda vitokanavyo na majeraha katika ngozi, kupasua vipele na chunusi. Ni utaratibu wa kawaida wa mwili kutengeneza seli mpya na vitu vingine vitakavyosaidia kukarabati sehemu ya mwili itakayopata majeraha. Ni kama sisi binadamu tunavyofanya kuziba viraka na viraka kuwa tofauti kidogo na sehemu zingine. Madoadoa na makovu hutofautiana rangi, ukubwa na kiasi gani yameingia ndani ya ngozi.