Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

RONALDO HAMTAKI KANE MADRID


Cristiano Ronaldo hayupo tayari kugawana umaarufu Real Madrid na nyota wa Tottenham, Harry Kane, kwa mujibu wa mchambuzi wa Sky Sports News Guillem Balague ( kupitia the Daily Star ).
Kane ameibuka kuwa shabaha ya miamba hao wa La Liga wanaohaha kutafuta kiwango chao cha msimu uliopita.
 
RONALDO HAMTAKI KANE MADRID


Cristiano Ronaldo hayupo tayari kugawana umaarufu Real Madrid na nyota wa Tottenham, Harry Kane, kwa mujibu wa mchambuzi wa Sky Sports News Guillem Balague ( kupitia the Daily Star ).
Kane ameibuka kuwa shabaha ya miamba hao wa La Liga wanaohaha kutafuta kiwango chao cha msimu uliopita.
 
BARCA YAANDAA FAGIO LA JANUARI


Barcelona inataka kusafisha kikosi chao dirisha la uhamisho Januari kwa kuwauza Arda Turan, Aleix Vidal na Thomas Vermaelen, kwa mujibu wa Sport.
Kocha Ernesto Valverde anataka kukisafisha kikosi chake kuelekea nusu ya pili ya msimu, na haitashangaza kuona Arda Turan na Vermaelen wakienguliwa.
Vidal naye amepoteza namba kufuatia ujio wa Nelson Semedo.
 
DE LIGT AINGIA KWENYE ORODHA YA BARCA


Barcelona wamemtaja beki kinda wa miaka 18 kutoka Ajax Matthijs de Ligt kuwa shabaha yao kuu uhamisho wa majira ya joto, kwa mujibu wa Mundo Deportivo .
Ripoti zinadai kuwa Blaugrana wanaamini kinda huyo wa kidachi ataendana na mfumo wao na atakuwa mchezaji mahiri zaidi siku za mbeleni.
 
EVERTON WANAMTAKA SIMEONE


Mmiliki wa Everton Farhad Moshiri anataka kumteua Diego Simeone kuwa meneja mpya wa klabu hiyo, kwa mujibu wa Sky Sports .
Kocha huyo mwenye njaa ya mafanikio anaweza kuondoka Atletico Madrid, miamba hao wa La Liga wanashika nafasi ya nne ligi ya Hispania na wapo katika hatari ya kutolewa Ligi ya Mabingwa.
 
BAYERN YAJIPANGA KUMSAJILI DRAXLER


Bayern Munich wanataka kumsajili mshambuliaji wa Paris Saint-Germain Julian Draxler mwisho wa msimu huu kuchukua nafasi ya Franck Ribery, kwa mujibu wa France Football .
Ribery anamaliza mkataba wake majira ya joto na Bayern hawajafanya uamuzi wa kumpa winga huyo mkataba mpya au la!
 
MAN UTD HAWATAMREJESHA PEREIRA


Valencia wanaamini Andreas Pereira hatarejeshwa Januari kwenye kikosi cha Manchester United, kwa hiyo wanataka kumsajili kwa mujibu wa Superdeporte .
United walikuwa na uwezo wa kusitisha mkataba wa mkopo wa Perera mwaka mpya, lakini winga huyo sasa anatarajiwa kumaliza kampeni hizi akiwa Valencia baada ya kung'ara La Liga.
 
NAVAS KUMRITHI CECH ARSENAL?


Arsenal inataka kumsajili kipa wa Real Madrid Keylor Navas kuwa mrithi wa Petr Cech, kwa mujibu wa Diario Gol .
Mustakabali wa Navas Madrid hauna uhakika kwani mchezaji huyo wa kimataifa wa Costa Rica imeripotiwa hana furaha kufuatia klabu hiyo kumfukuzia David de Gea wa Manchester United.
 
MONACO & BARCA ZILIFIKIA MAKUBALIANO YA MBAPPE


Barcelona na Monaco zilikubaliana uhamisho wa Kylian Mbappe kabla ya kinda huyo kuamua kujiunga na Paris Saint-Germain, kwa mujibu wa L'Equipe .
Mpango huo wa kumsajili Mbappe ungetimia, Arda Turan angejiunga na Monaco, lakini kinda huyo wa Kifaransa alikataa.
 
CHELSEA YAFIKIRIA KUMSAJILI DIAKHABY


Chelsea wanafikiria kumsajili beki mahiri wa Lyon, Mouctar Diakhaby, kwa mujibu wa Daily Mail .
Mchezaji huyo wa timu ya Ufaransa umri chini ya miaka 21 amekuwa katika kiwango bora kwenye ligi ya Ufaransa msimu huu.
 
Back
Top Bottom